Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -




Isaya 29:15 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC

15 Ole wao wanaojitahidi kumficha BWANA mashauri yao, na matendo yao yamo gizani, nao husema, Ni nani atuonaye? Nani atujuaye?

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

15 “Ole mnaomficha Mwenyezi-Mungu mipango yenu, mnaotenda matendo yenu gizani na kusema: ‘Hamna atakayetuona; nani awezaye kujua tunachofanya?’

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

15 “Ole mnaomficha Mwenyezi-Mungu mipango yenu, mnaotenda matendo yenu gizani na kusema: ‘Hamna atakayetuona; nani awezaye kujua tunachofanya?’

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

15 “Ole mnaomficha Mwenyezi-Mungu mipango yenu, mnaotenda matendo yenu gizani na kusema: ‘Hamna atakayetuona; nani awezaye kujua tunachofanya?’

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

15 Ole kwa wale wanaoenda kwenye vilindi virefu kumficha Mwenyezi Mungu mipango yao, wafanyao kazi zao gizani na kufikiri, “Ni nani anayetuona? Ni nani atakayejua?”

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

15 Ole kwa wale wanaokwenda kwenye vilindi virefu kumficha bwana mipango yao, wafanyao kazi zao gizani na kufikiri, “Ni nani anayetuona? Ni nani atakayejua?”

Tazama sura Nakili




Isaya 29:15
30 Marejeleo ya Msalaba  

Hata maombolezo hayo yalipokwisha, Daudi akatuma mtu, akamtwaa, akamtia nyumbani mwake; naye akawa mkewe, akamzalia mtoto wa kiume. Lakini jambo lile alilolitenda Daudi likamchukiza BWANA.


Tena, wana wa Israeli wakafanya kwa siri mambo yasiyokuwa mema juu ya BWANA, Mungu wao, wakajijengea mahali pa juu katika miji yao yote, kutoka mnara wa walinzi hata katika miji yenye boma.


Hapana hofu ya giza kuu, mahali wawezapo kujificha watendao udhalimu.


Tazama, kwa vinywa vyao huteuka, Midomoni mwao mna panga, Kwa maana ni nani asikiaye?


Nao husema, Mungu ajuaje? Yako maarifa kwake aliye juu?


Juu ya watu wako wanafanya hila, Na kushauriana juu yao uliowaficha.


Kwa sababu mmesema, Tumefanya agano na mauti, tumepatana na kuzimu; pigo lifurikalo litakapopita, halitatufikia sisi; kwa maana tumefanya maneno ya uongo kuwa kimbilio letu, tumejificha chini ya maneno yasiyo kweli;


Nami nitafanya hukumu kuwa ndiyo kanuni, na haki kuwa ndiyo timazi; na mvua ya mawe itachukulia mbali hilo kimbilio la maneno ya uongo, na maji yatapagharikisha mahali pa kujisitiri.


Ole wa watoto waasi; asema BWANA; watakao mashauri lakini hawayataki kwangu mimi; wajifunikao kifuniko lakini si cha roho yangu; wapate kuongeza dhambi juu ya dhambi;


Maana umeutumainia ubaya wako; umesema, Hapana anionaye; hekima yako, na maarifa yako yamekupotosha, nawe umesema moyoni mwako, Mimi ndiye, wala hapana mwingine zaidi yangu mimi.


Mimi nitatangaza haki yako, na matendo yako hayatakufaa.


Je, mtu yeyote aweza kujificha mahali pa siri, nisimwone? Asema BWANA. Je! Mbingu na nchi hazikujawa nami? Asema BWANA.


Kisha akaniambia, Mwanadamu, umeyaona wanayotenda wazee wa nyumba ya Israeli gizani, kila mtu ndani ya vyumba vyake vya sanamu? Maana husema, BWANA hatuoni; BWANA ameiacha nchi hii.


Ndipo akaniambia, Mwanadamu, toboa sasa katika ukuta huu; nami nilipotoboa, tazama, pana mlango.


Ndipo akaniambia, Uovu wa nyumba ya Israeli na Yuda ni mwingi sana, nayo nchi imejaa damu, nao mji umejaa kupotosha hukumu; maana husema, BWANA ameiacha nchi hii, naye BWANA haoni.


Nao walioasi wameongeza sana ufisadi wao; lakini mimi ndiye awakaripiaye wote pia.


Kisha itakuwa wakati ule, nitauchunguza Yerusalemu kwa taa; nami nitawaadhibu watu walioganda juu ya masira yao; wasemao katika mioyo yao, BWANA hatatenda mema, wala hatatenda mabaya.


Mmemchokesha BWANA kwa maneno yenu. Lakini ninyi mwasema, Tumemchokesha kwa maneno gani? Kwa kuwa mwasema, Kila atendaye mabaya ni mwema machoni pa BWANA, naye huwafurahia watu hao, au, Mungu mwenye haki yuko wapi?


Na hii ndiyo hukumu; ya kuwa nuru imekuja ulimwenguni, na watu wakapenda giza kuliko nuru; kwa maana matendo yao yalikuwa maovu.


Basi ninyi msihukumu neno kabla ya wakati wake, hata ajapo Bwana; ambaye atayamulika yaliyositirika katika giza, na kuyadhihirisha mashauri ya mioyo; ndipo kila mtu atakapoipata sifa yake kwa Mungu.


lakini tumekataa mambo ya aibu yaliyositirika, wala hatuenendi kwa hila, wala kulichanganya neno la Mungu na uongo; bali kwa kuidhihirisha iliyo kweli twajionesha kuwa na haki, dhamiri za watu zikitushuhudia mbele za Mungu.


nami nitawaua watoto wake kwa mauti. Na makanisa yote watajua ya kuwa mimi ndiye achunguzaye fikira na mioyo. Nami nitampa kila mmoja wenu kwa kadiri ya matendo yake.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo