Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -




Isaya 29:14 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC

14 kwa sababu hiyo mimi nitafanya tena kazi ya ajabu kati ya watu hawa, kazi ya ajabu na mwujiza; na akili za watu wao wenye akili zitapotea, na ufahamu wa wenye busara wao utafichwa.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

14 Hivyo, nitawatenda tena watu hawa maajabu, mambo ya ajabu na ya kushangaza. Nao wenye hekima wao wataishiwa hekima, na busara ya wenye busara wao itatoweka.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

14 Hivyo, nitawatenda tena watu hawa maajabu, mambo ya ajabu na ya kushangaza. Nao wenye hekima wao wataishiwa hekima, na busara ya wenye busara wao itatoweka.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

14 Hivyo, nitawatenda tena watu hawa maajabu, mambo ya ajabu na ya kushangaza. Nao wenye hekima wao wataishiwa hekima, na busara ya wenye busara wao itatoweka.”

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

14 Kwa hiyo mara nyingine tena nitawashangaza watu hawa, kwa ajabu juu ya ajabu. Hekima ya wenye hekima itapotea, nayo akili ya wenye akili itatoweka.”

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

14 Kwa hiyo mara nyingine tena nitawashangaza watu hawa, kwa ajabu juu ya ajabu. Hekima ya wenye hekima itapotea, nayo akili ya wenye akili itatoweka.”

Tazama sura Nakili




Isaya 29:14
24 Marejeleo ya Msalaba  

Yeye huwaondoa washauri wakiwa wamevuliwa nguo, Naye huwafanya waamuzi kuwa ni wapumbavu.


Yeye huwanasa wenye hekima katika hila yao wenyewe; Na mashauri ya washupavu yaharibika kwa haraka.


Basi, itakuwa, Bwana atakapokuwa ameitimiza kazi yake yote juu ya mlima Sayuni na juu ya Yerusalemu, nitamwadhibu matunda ya kiburi cha moyo wake mfalme wa Ashuru, na majivuno ya macho yake.


Na roho yao Misri itaondolewa, nami nitaiharibu mipango yao, nao watakwenda kwa sanamu zao, na kwa waganga, na kwa wapiga ramli na kwa wachawi.


Maana BWANA ataondoka kama vile katika mlima Perasimu, ataghadhibika kama vile katika bonde la Gibeoni; apate kufanya kazi yake, kazi yake ya ajabu; na kulitimiza tendo lake, tendo lake la ajabu.


Nizitanguaye ishara za waongo, na kuwatia waganga wazimu; niwarudishaye nyuma wenye hekima, na kuyageuza maarifa yao kuwa ujinga;


Ee BWANA, mbona umetukosesha njia zako, ukatufanya kuwa na mioyo migumu hata tusikuogope? Urudi kwa ajili ya watumishi wako, makabila ya urithi wako.


maovu yenu na maovu ya baba zenu pamoja, asema BWANA, ninyi mliofukiza uvumba juu ya milima, na kunitukana juu ya vilima; basi, kwa ajili ya hayo nitawapimia kwanza kazi yao vifuani mwao.


Nami nitalitangua shauri la Yuda na Yerusalemu mahali hapa; nami nitawaangusha kwa upanga mbele za adui zao, na kwa mkono wa watu watafutao roho zao; na mizoga yao nitawapa ndege wa angani na wanyama wakali wa nchi, iwe chakula chao.


Kuhusu Edomu. BWANA wa majeshi asema hivi, Je! Hakuna tena hekima katika Temani? Mashauri yamewapotea wenye busara? Je! Imetoweka hekima yao?


Siku hiyo, je! Sitawaangamiza watu wenye akili katika Edomu, na wenye ufahamu katika kilima cha Esau? Asema BWANA.


Angalieni, enyi mlio kati ya mataifa, katazameni, kastaajabuni sana; kwa maana mimi natenda tendo siku zenu, ambalo hamtaliamini hata mkiambiwa.


Kwa kuwa nawaambia ya kwamba manabii wengi na wafalme walitamani kuyaona mnayoyaona ninyi wasiyaone; na kuyasikia mnayoyasikia ninyi wasiyasikie.


Na kama walivyokataa kuwa na Mungu katika fahamu zao, Mungu aliwaacha wafuate akili zao zisizofaa, wayafanye yasiyowapasa.


Maana hekima ya dunia hii ni upuzi mbele za Mungu. Kwa maana imeandikwa, Yeye ndiye awanasaye wenye hekima katika hila yao.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo