Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -




Isaya 28:29 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC

29 Hayo nayo yatoka kwa BWANA wa majeshi, mwenye shauri la ajabu, apitaye wote kwa hekima yake.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

29 Ujuzi huu nao watoka kwa Mwenyezi-Mungu wa majeshi. Mipango yake Mungu ni ya ajabu, hekima yake ni kamilifu kabisa.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

29 Ujuzi huu nao watoka kwa Mwenyezi-Mungu wa majeshi. Mipango yake Mungu ni ya ajabu, hekima yake ni kamilifu kabisa.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

29 Ujuzi huu nao watoka kwa Mwenyezi-Mungu wa majeshi. Mipango yake Mungu ni ya ajabu, hekima yake ni kamilifu kabisa.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

29 Haya yote pia hutoka kwa Mwenyezi Mungu, Mungu wa majeshi ya mbinguni, mwenye mashauri ya ajabu, na anayepita wote kwa hekima.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

29 Haya yote pia hutoka kwa bwana Mwenye Nguvu Zote, mwenye mashauri ya ajabu, na anayepita wote kwa hekima.

Tazama sura Nakili




Isaya 28:29
15 Marejeleo ya Msalaba  

Yeye Mwenyezi hamwezi kumwona; Yeye ni mkuu mwenye uweza; Tena mwenye hukumu, na mwingi wa haki, hataonea.


Yeye afanyaye mambo makuu, yasiyotambulikana; Mambo ya ajabu yasiyo na hesabu;


Neno hili limetoka kwa BWANA, Nalo ni ajabu machoni petu.


Ee BWANA, Mungu wangu, umefanya kwa wingi Miujiza yako na mawazo yako kwetu; Hakuna awezaye kufananishwa nawe; Kama ningependa kuyatangaza na kuyahubiri, Ni mengi sana hayahesabiki.


Ee BWANA, jinsi yalivyo makuu matendo yako! Mawazo yako ni mafumbo makubwa.


Mtu mjinga hayatambui hayo, Wala mpumbavu hayafahamu.


Ushauri ni wangu, na maarifa yaliyo sahihi; Mimi ni ufahamu, mimi nina nguvu.


Ngano ya mkate husagwa; kwa maana haipuri siku zote bila kukoma; na ingawa gurudumu la gari lake na farasi wake huitawanya ngano ile, haisagi.


Lakini yeye naye ana akili, naye ataleta uovu, wala hatayatangua maneno yake; bali ataondoka juu ya nyumba yao watendao mabaya, na juu ya msaada wa hao watendao maovu.


ili waone, na kujua, wakafikiri, na kufahamu pamoja, ya kuwa mkono wa BWANA ndio uliofanya jambo hilo. Mtakatifu wa Israeli ndiye aliyeliumba.


Maana kwa ajili yetu mtoto amezaliwa, Tumepewa mtoto wa kiume; Na uweza wa kifalme utakuwa begani mwake; Naye ataitwa jina lake, Mshauri wa Ajabu, Mungu Mwenye Nguvu, Baba wa Milele, Mfalme wa Amani.


mkuu wa mashauri, muweza katika kutenda; ambaye macho yake yamefumbuka juu ya njia zote za wanadamu, kumpa kila mtu kwa kadiri ya njia zake, na kwa kadiri ya matunda ya matendo yake,


Jinsi zilivyo kuu utajiri na hekima na maarifa ya Mungu! Hukumu zake hazichunguziki, wala njia zake hazieleweki!


Tufuate:

Matangazo


Matangazo