Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -




Isaya 28:27 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC

27 Kwa maana kunde zile hazipurwi kwa chombo kikali, wala gurudumu la gari halipitishwi huku na huko juu ya jira ile, bali kunde zile hupurwa kwa fimbo, na jira ile kwa ufito.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

27 Bizari haipurwi kwa mtarimbo wala jira kwa gari la ng'ombe! Ila bizari hupurwa kwa kijiti na jira kwa fimbo.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

27 Bizari haipurwi kwa mtarimbo wala jira kwa gari la ng'ombe! Ila bizari hupurwa kwa kijiti na jira kwa fimbo.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

27 Bizari haipurwi kwa mtarimbo wala jira kwa gari la ng'ombe! Ila bizari hupurwa kwa kijiti na jira kwa fimbo.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

27 Iliki haipurwi kwa nyundo, wala gurudumu la gari halivingirishwi juu ya jira; iliki hupurwa kwa fimbo, na jira kwa ufito.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

27 Iliki haipurwi kwa nyundo, wala gurudumu la gari halivingirishwi juu ya jira; iliki hupurwa kwa fimbo, na jira kwa ufito.

Tazama sura Nakili




Isaya 28:27
10 Marejeleo ya Msalaba  

Kwa kuwa hakumwachia Yehoahazi watu ila wapandao farasi hamsini, na magari kumi, na askari elfu kumi waendao kwa miguu; kwa kuwa mfalme wa Shamu aliwaharibu, akawaponda mfano wa mavumbi yaliyokanyagwa.


Mfalme mwenye hekima huwapepeta wasio haki; Naye hulipitisha gurudumu la kupuria juu yao.


Kwa maana Mungu wake anamwagiza vizuri na kumfundisha.


Ngano ya mkate husagwa; kwa maana haipuri siku zote bila kukoma; na ingawa gurudumu la gari lake na farasi wake huitawanya ngano ile, haisagi.


Tazama, nitakufanya kuwa chombo kikali kipya cha kupuria, chenye meno; utaifikicha milima, na kuisaga; nawe utafanya vilima kuwa kama makapi.


Ee BWANA, unirudi kwa haki; si kwa hasira yako, usije ukaniangamiza.


Usiogope wewe, Ee Yakobo, mtumishi wangu, asema BWANA; kwa maana mimi ni pamoja nawe; maana nitawakomesha kabisa mataifa yote huko nilikokufukuza, bali sitakukomesha wewe kabisa; lakini nitakurudi kwa hukumu, wala sitakuacha bila adhabu.


Haya ndiyo asemayo BWANA; Kwa makosa matatu ya Dameski, naam, kwa manne, sitaizuia adhabu yake isimpate; kwa sababu wameipura Gileadi kwa vyombo vya kupuria vya chuma;


Ole wenu Waandishi na Mafarisayo, wanafiki! Kwa kuwa mnalipa zaka za mnanaa, bizari na jira, lakini mmeacha mambo makuu ya sheria, yaani, adili, na rehema, na imani; hayo imewapasa kuyafanya, wala yale mengine msiyaache.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo