Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -




Isaya 14:32 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC

32 Wajumbe wa taifa hilo waletewe jibu gani? Ya kuwa BWANA ameiweka misingi ya Sayuni, na ndani yake wale walioonewa katika watu wake watapata kimbilio kwake.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

32 Basi watapewa jibu gani wajumbe wa taifa hilo? Wataambiwa: Mwenyezi-Mungu ameijenga imara Siyoni, na maskini wa watu wake watakimbilia usalama huko.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

32 Basi watapewa jibu gani wajumbe wa taifa hilo? Wataambiwa: Mwenyezi-Mungu ameijenga imara Siyoni, na maskini wa watu wake watakimbilia usalama huko.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

32 Basi watapewa jibu gani wajumbe wa taifa hilo? Wataambiwa: Mwenyezi-Mungu ameijenga imara Siyoni, na maskini wa watu wake watakimbilia usalama huko.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

32 Ni jibu gani litakalotolewa kwa wajumbe wa taifa hilo? “Mwenyezi Mungu ameifanya imara Sayuni, na ndani yake watu wake walioonewa watapata kimbilio.”

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

32 Ni jibu gani litakalotolewa kwa wajumbe wa taifa hilo? “bwana ameifanya imara Sayuni, nako ndani yake watu wake walioonewa watapata kimbilio.”

Tazama sura Nakili




Isaya 14:32
30 Marejeleo ya Msalaba  

Tou akamtuma Yoramu mwanawe kwa mfalme Daudi ili kumsalimia, na kumpongeza, na kumbariki, kwa sababu amepigana na Hadadezeri, na kumpiga; kwa maana Hadadezeri alikuwa amepigana vita juu ya Tou. Na mkononi mwake Yorabu akaleta vyombo vya fedha, na vyombo vya dhahabu, na vyombo vya shaba;


BWANA atakapokuwa ameijenga Sayuni, Atakapoonekana katika utukufu wake,


Wana wa watumishi wako watakaa, Na wazawa wao wataimarishwa mbele zako.


Maana, tazama, wafalme walikusanyika; Walikuja wote pamoja.


Msingi wake upo Juu ya milima mitakatifu.


Naam, kuhusu Sayuni yatasemwa, Huyu na huyu alizaliwa humo. Na Yeye Aliye Juu Atauimarisha.


Jina la BWANA ni ngome imara; Mwenye haki huikimbilia, akawa salama.


bali kwa haki atawahukumu maskini, naye atawaonya wanyenyekevu wa dunia kwa adili; naye ataipiga dunia kwa fimbo ya kinywa chake, na kwa pumzi ya midomo yake atawaua wabaya.


Paza sauti, piga kelele, mwenyeji wa Sayuni; Maana Mtakatifu wa Israeli ni mkuu kati yako.


Maana umekuwa ngome ya maskini, Ngome ya mhitaji katika dhiki yake, Mahali pa kukimbilia wakati wa tufani, Na kivuli wakati wa joto; Wakati kishindo cha watu wakatili kilipokuwa, Kama dhoruba ipigayo ukuta.


kwa ajili ya hayo Bwana, MUNGU, asema hivi, Tazama, naweka jiwe katika Sayuni, liwe msingi, jiwe lililojaribiwa, jiwe la pembeni lenye thamani, msingi ulio imara; yeye aaminiye hatafanya haraka.


Wanyenyekevu nao wataongeza furaha yao katika BWANA, na maskini katika wanadamu watafurahi katika Mtakatifu wa Israeli.


Maana katika Yerusalemu yatatoka mabaki, nao watakaookoka katika mlima Sayuni; wivu wa BWANA wa majeshi utatimiza mambo hayo.


Naye alisikia habari ya Tirhaka, mfalme wa Kushi, ya kwamba, Ametoka ili kupigana nawe; naye aliposikia hayo, akatuma wajumbe kwa Hezekia, kusema,


Wakati huo Merodak-baladani, mwana wa Baladani, mfalme wa Babeli, alipeleka barua na zawadi kwa Hezekia; kwa maana amepata habari kwamba amekuwa mgonjwa, na kwamba amepona.


Kisha kutakuwa na hema kuwa uvuli wakati wa mchana kwa sababu ya joto, na kuwa mahali pa kukimbilia na kujificha wakati wa tufani na mvua.


nimwambiaye Koreshi, Mchungaji wangu, naye atayatenda mapenzi yangu; hata ataunena Yerusalemu, Utajengwa; na hilo hekalu, Msingi wako utawekwa.


Ewe uliyeteswa, uliyerushwa na tufani, usiyetulizwa, tazama, nitaweka mawe yako kwa rangi nzuri, nitaweka misingi yako kwa yakuti samawi.


Utakapolia, na wakuponye hao uliowakusanya; lakini upepo utawachukua; uvuvio tu utawachukulia mbali; lakini yeye anayenitumaini ataimiliki nchi, na kuurithi mlima wangu mtakatifu.


Kuuzunguka ni mianzi elfu kumi na nane; na jina la mji huo tangu siku hiyo litakuwa hili, BWANA yupo.


Lakini nitabakiza ndani yako watu walioonewa na maskini, nao watalitumainia jina la BWANA.


Nayo ikavunjwa siku ile; na hivyo wale kondoo wanyonge walionisikiliza wakajua ya kuwa neno hili ndilo neno la BWANA.


Basi nikalilisha kundi la machinjo, kweli kondoo waliokuwa wanyonge kabisa. Kisha nikajipatia fimbo mbili; nami nikaiita ya kwanza, Neema, na ya pili nikaiita, Umoja; nikalilisha kundi lile.


Nami nakuambia, Wewe ndiwe Petro, na juu ya mwamba huu nitalijenga kanisa langu; wala milango ya kuzimu haitalishinda.


Maana alikuwa akiutazamia mji wenye misingi, ambao mwenye kuubuni na kuujenga ni Mungu.


Bali ninyi mmeufikia mlima Sayuni, na mji wa Mungu aliye hai, Yerusalemu wa mbinguni, na majeshi ya malaika elfu nyingi,


Ndugu zangu wapenzi, sikilizeni, Je! Mungu hakuwachagua maskini wa dunia wawe matajiri wa imani na warithi wa ufalme aliowaahidia wampendao?


Tufuate:

Matangazo


Matangazo