Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -




Isaya 14:19 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC

19 Bali wewe umetupwa mbali na kaburi lako, Kama chipukizi lililochukiza kabisa; Kama vazi la wale waliouawa, Wale waliochomwa kwa upanga, Wale washukao mpaka misingi ya shimo; Kama mzoga uliokanyagwa chini ya miguu.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

19 Lakini wewe umetupwa nje ya kaburi lako; kama mtoto wa kuchukiza aliyezaliwa mfu maiti yako imekanyagwakanyagwa, umerundikiwa maiti za waliouawa kwa upanga, waliotupwa mashimoni penye mawe.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

19 Lakini wewe umetupwa nje ya kaburi lako; kama mtoto wa kuchukiza aliyezaliwa mfu maiti yako imekanyagwakanyagwa, umerundikiwa maiti za waliouawa kwa upanga, waliotupwa mashimoni penye mawe.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

19 Lakini wewe umetupwa nje ya kaburi lako; kama mtoto wa kuchukiza aliyezaliwa mfu maiti yako imekanyagwakanyagwa, umerundikiwa maiti za waliouawa kwa upanga, waliotupwa mashimoni penye mawe.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

19 Lakini wewe umetupwa nje ya kaburi lako kama tawi lililokataliwa, umefunikwa na waliouawa pamoja na wale waliochomwa kwa upanga, wale wanaoshuka hadi kwenye mawe ya shimo. Kama mzoga uliokanyagwa chini ya nyayo,

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

19 Lakini wewe umetupwa nje ya kaburi lako kama tawi lililokataliwa, umefunikwa na waliouawa pamoja na wale waliochomwa kwa upanga, wale washukao mpaka kwenye mawe ya shimo. Kama mzoga uliokanyagwa chini ya nyayo,

Tazama sura Nakili




Isaya 14:19
17 Marejeleo ya Msalaba  

Ukamwambie, ukisema, BWANA asema hivi, Je! Umeua, ukatamalaki? Nawe utamwambia, kusema, BWANA asema hivi, Mahali pale mbwa walipoiramba damu ya Nabothi, mbwa watairamba na damu yako, naam, damu yako.


Mtu wa nyumba ya Ahabu afaye mjini, mbwa watamla, na yeye afaye mashambani ndege wa angani watamla.


Ndipo Yehu akamwambia Bidkari, msaidizi wake, Mtwae ukamtupe katika kiwanja cha Nabothi, Myezreeli; maana kumbuka, hapo mimi na wewe tulipokuwa tumepanda farasi zetu, na kumfuata Anabu baba yake, BWANA alimwekea mzigo huu, akasema;


Kila mtu atakayeonekana atatumbuliwa, na kila mtu atakayepatikana ataanguka kwa upanga.


Wafalme wote wa mataifa wamezikwa wote kwa heshima, Kila mmoja ndani ya nyumba yake mwenyewe;


Watu wao waliouawa watatupwa nje, na uvundo wa maiti zao utapaa juu, na milima itayeyushwa kwa damu yao.


Kwa sababu hiyo hasira ya BWANA imewaka juu ya watu wake, naye amenyosha mkono wake juu yao; akawapiga, navyo vilima vilitetemeka, na mizoga yao ilikuwa kama takataka katika njia kuu. Pamoja na hayo yote hasira yake haikugeukia mbali, lakini mkono wake umenyoshwa hata sasa.


Wakubwa kwa wadogo wote pia watakufa katika nchi hii; hawatazikwa, wala watu hawatawalilia, wala kujikatakata kwa ajili yao, wala kujinyoa kwa ajili yao;


Atazikwa maziko ya punda, akibururwa, na kutupwa nje ya malango ya Yerusalemu.


Basi ikawa walipokuwa katikati ya mji, Ishmaeli, mwana wa Nethania, akawaua, akawatupa katika shimo, yeye na watu wale waliokuwa pamoja naye.


Basi, shimo lile, ambalo Ishmaeli amezitupa maiti za watu aliowaua, karibu na Gedalia, (ni lile lile alilolichimba Asa, mfalme, kwa kuwa alimwogopa Baasha, mfalme wa Israeli), Ishmaeli, mwana wa Nethania, akalijaza kwa watu wale aliowaua.


Nao wataanguka, wakiwa wameuawa, katika nchi ya Wakaldayo, wakiwa wametumbuliwa katika njia zake kuu.


ambao makaburi yao yamewekwa pande za shimo zilizo mbali sana, umati wote wamezunguka kaburi lake; wote pia wameuawa, wameanguka kwa upanga, waliotisha katika nchi yao walio hai.


Je! Wasilale pamoja na mashujaa wao wasiotahiriwa, walioanguka, walioshuka kuzimu pamoja na silaha zao za vita, ambao wameweka panga zao chini ya vichwa vyao, na maovu yao mifupani mwao? Maana waliwatisha mashujaa katika nchi ya walio hai.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo