Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Hosea 10:9 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC

9 Ee Israeli, umefanya dhambi tangu siku za Gibea; huko ndiko walikosimama; Je, vita juu ya wana wa uovu hakitawapata katika Gibea?

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

9 Enyi Waisraeli, nyinyi mmetenda dhambi tangu kule Gibea, na bado mnaendelea. Hakika vita vitawaangamiza hukohuko Gibea.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

9 Enyi Waisraeli, nyinyi mmetenda dhambi tangu kule Gibea, na bado mnaendelea. Hakika vita vitawaangamiza hukohuko Gibea.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

9 Enyi Waisraeli, nyinyi mmetenda dhambi tangu kule Gibea, na bado mnaendelea. Hakika vita vitawaangamiza hukohuko Gibea.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

9 “Tangu siku za Gibea, umetenda dhambi, ee Israeli, huko ndiko ulibaki. Je, vita havikuwapata watenda maovu huko Gibea?

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

9 “Tangu siku za Gibea, mmetenda dhambi, ee Israeli, huko ndiko mlikobaki. Je, vita havikuwapata watenda mabaya huko Gibea?

Tazama sura Nakili




Hosea 10:9
12 Marejeleo ya Msalaba  

BWANA akaona ya kuwa maovu ya mwanadamu ni makubwa duniani na kwamba kila kusudi analowaza moyoni mwake ni baya tu siku zote.


BWANA akasikia harufu ya kumridhisha; BWANA akasema moyoni, Sitailaani nchi tena baada ya hayo kwa sababu ya wanadamu, maana mawazo ya moyo wa mwanadamu ni mabaya tangu ujana wake; wala sitapiga tena baada ya hayo kila kilicho hai kama nilivyofanya. 1


Wakati nitakapopenda nitawaadhibu; na hao mataifa watakusanyika juu yao, watakapofungwa kwa sababu ya makosa yao mawili.


Mahali pa Aveni palipoinuka, yaani, dhambi ya Israeli, pataharibika; mwiba na mbigili itamea juu ya madhabahu zake; nao wataiambia milima, Tusitirini; na vilima, Tuangukieni.


Pigeni tarumbeta katika Gibea, na baragumu katika Rama; pazeni sauti ya hofu katika Beth-aveni; nyuma yako, Ee Benyamini!


Wamejiharibu mno, kama katika siku za Gibea; ataukumbuka uovu wao, atazilipiza dhambi zao.


Nao wanaume wa Gibea wakaniondokea, na kuizingira hiyo nyumba pande zote juu yangu wakati wa usiku; walitaka kuniua, na suria wangu wakambaka nguvu, hata amekufa.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo