Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -




Hesabu 35:34 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC

34 Kwa hiyo msiitie unajisi nchi mwishiyo ambayo nami nakaa kati yake; kwa kuwa mimi BWANA nakaa kati ya wana wa Israeli.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

34 Msiitie unajisi nchi ambayo mnakaa, nchi ambayo mimi ninakaa; maana mimi Mwenyezi-Mungu ninakaa miongoni mwenu Waisraeli.”

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

34 Msiitie unajisi nchi ambayo mnakaa, nchi ambayo mimi ninakaa; maana mimi Mwenyezi-Mungu ninakaa miongoni mwenu Waisraeli.”

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

34 Msiitie unajisi nchi ambayo mnakaa, nchi ambayo mimi ninakaa; maana mimi Mwenyezi-Mungu ninakaa miongoni mwenu Waisraeli.”

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

34 Msiinajisi nchi mnayoishi, ambayo nami ninakaa, kwa kuwa Mimi, Mwenyezi Mungu, ninakaa katikati ya Waisraeli.’ ”

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

34 Msiinajisi nchi mnayoishi, ambayo nami ninakaa, kwa kuwa Mimi, bwana, ninakaa katikati ya Waisraeli.’ ”

Tazama sura Nakili




Hesabu 35:34
20 Marejeleo ya Msalaba  

Nami nitakaa katikati ya wana wa Israeli, wala sitawaacha watu wangu Israeli.


Hapo ndipo mahali pangu pa raha milele, Hapo nitakaa kwa maana nimepatamani.


Na ahimidiwe BWANA toka Sayuni, Akaaye Yerusalemu. Haleluya.


Nao na wanifanyie patakatifu; ili nipate kukaa kati yao.


Maana yeye aliye juu, aliyetukuka, akaaye milele; ambaye jina lake ni Mtakatifu; asema hivi; Nakaa mimi mahali palipoinuka, palipo patakatifu; tena pamoja na yeye aliye na roho iliyotubu na kunyenyekea, ili kuzifufua roho za wanyenyekevu, na kuifufua mioyo yao waliotubu.


Msiseme, Ni njama, kuhusu mambo yote ambayo watu hawa watasema, Ni njama; msihofu kwa hofu yao, wala msiogope.


Nami kwanza nitawalipa uovu wao na dhambi zao maradufu, kwa kuwa wameitia unajisi nchi yangu, kwa mizoga ya vitu vyao vichukizavyo, na kuujaza urithi wangu kwa machukizo yao.


Kwa sababu umesema, Mataifa haya mawili na nchi hizi mbili zitakuwa zangu, nasi tutazimiliki, ijapokuwa BWANA alikuwako huko.


Hawatakaa katika nchi ya BWANA; lakini Efraimu atarudi Misri, nao watakula chakula najisi katika Ashuru.


nao wakakusanyika kinyume cha Musa na Haruni, na kuwaambia, Ninyi inawatosha, kwa kuwa mkutano wote ni mtakatifu, kila mmoja miongoni mwao, BWANA naye yuko kati yao; ya nini basi kujitukuza juu ya mkutano wa BWANA?


mtawatoa nje wote, wanaume kwa wanawake, mtawaweka nje ya kambi; ili wasizitie unajisi kambi zao, ambazo mimi naketi katikati yazo.


mzoga wake usikae usiku kucha juu ya mti; lazima utamzika siku iyo hiyo; kwani aliyetundikwa amelaaniwa na Mungu; usije ukatia unajisi katika nchi yako akupayo BWANA, Mungu wako, iwe urithi wako.


Ee BWANA, wasamehe watu wako Israeli, uliowakomboa, wala usiiache damu ya asiye makosa ikakaa katikati ya watu wako Israeli. Na ile damu utasamehewa kwao.


kwani BWANA, Mungu wako, aliye katikati yako ni Mungu mwenye wivu; isije ikawaka juu yako hasira ya BWANA, Mungu wako, akakuangamiza kutoka juu ya uso wa nchi.


Na ndani yake hakitaingia kamwe chochote kilicho kinyonge, wala yeye afanyaye machukizo na uongo, bali wale walioandikwa katika kitabu cha uzima cha Mwana-kondoo.


Nikasikia sauti kubwa kutoka katika kile kiti cha enzi ikisema, Tazama, maskani ya Mungu ni pamoja na wanadamu, naye atafanya maskani yake pamoja nao, nao watakuwa watu wake. Naye Mungu mwenyewe atakuwa pamoja nao.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo