Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -




Hesabu 35:25 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC

25 nao mkutano utamwokoa yule aliyemwua mtu na mkono wa mwenye kulipiza kisasi cha damu; tena mkutano utamrejesha katika mji wake wa makimbilio, aliokuwa anaukimbilia; naye atakaa humo hata kifo chake kuhani mkuu, aliyepakwa mafuta matakatifu.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

25 Jumuiya itamwokoa mtu huyo aliyeua mikononi mwa jamaa ya mtu aliyeuawa, na kumrudisha katika mji wa makimbilio alimokuwa amekimbilia. Atakaa huko mpaka kifo cha kuhani mkuu wa wakati huo aliyeteuliwa kwa kupakwa mafuta matakatifu.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

25 Jumuiya itamwokoa mtu huyo aliyeua mikononi mwa jamaa ya mtu aliyeuawa, na kumrudisha katika mji wa makimbilio alimokuwa amekimbilia. Atakaa huko mpaka kifo cha kuhani mkuu wa wakati huo aliyeteuliwa kwa kupakwa mafuta matakatifu.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

25 Jumuiya itamwokoa mtu huyo aliyeua mikononi mwa jamaa ya mtu aliyeuawa, na kumrudisha katika mji wa makimbilio alimokuwa amekimbilia. Atakaa huko mpaka kifo cha kuhani mkuu wa wakati huo aliyeteuliwa kwa kupakwa mafuta matakatifu.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

25 Kusanyiko lazima wamlinde yule anayeshtakiwa kuua kutoka kwa mlipiza kisasi wa damu, na kumrudisha katika mji wa makimbilio alikokuwa amekimbilia. Lazima akae humo hadi atakapokufa kuhani mkuu aliyekuwa amepakwa mafuta matakatifu.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

25 Kusanyiko ni lazima limlinde yule anayeshtakiwa kuua kutoka kwa mlipiza kisasi wa damu, na kumrudisha katika mji wa makimbilio alikokuwa amekimbilia. Lazima akae humo mpaka atakapokufa kuhani mkuu ambaye alikuwa amepakwa mafuta matakatifu.

Tazama sura Nakili




Hesabu 35:25
15 Marejeleo ya Msalaba  

Kwa kuwa hatuna budi kufa, nasi tu kama maji yaliyomwagika chini, yasiyoweza kuzoleka tena; wala Mungu haondoi maisha ila hufikiri shauri, kwamba yeye aliyefukuzwa asiwe mkimbizi kwake.


Ndipo utakapotwaa hayo mafuta ya kupaka, na kummiminia kichwani mwake, na kumtia mafuta.


Na yeye aliye kuhani mkuu katika nduguze, ambaye mafuta ya kutiwa yamemiminwa kichwani mwake, naye akawekwa wakfu ili ayavae hayo mavazi, yeye hataziacha wazi nywele za kichwa chake, wala hatazirarua nguo zake;


kama kuhani aliyetiwa mafuta akifanya dhambi, hata analeta hatia juu ya watu; ndipo na atoe kwa ajili ya dhambi yake aliyoifanya, na kumsongeza kwa BWANA ng'ombe dume mchanga mkamilifu, kuwa ni sadaka ya dhambi.


Kisha akamimina mafuta hayo ya kutia kichwani mwake Haruni, na kumtia mafuta, ili amtakase.


ndipo mkutano utaamua kati ya huyo aliyempiga mtu na huyo atakayelipiza kisasi cha damu, kama hukumu hizi zilivyo;


Lakini kama mwenye kumwua mtu akienda wakati wowote kupita mpaka wa huo mji wa makimbilio, alioukimbilia;


kwa sababu ilimpasa kukaa ndani ya mji wake wa makimbilio hadi kifo chake kuhani mkuu lakini kuhani mkuu atakapokwisha kufa huyo mwuaji atarudi aende nchi ya urithi wake.


Naye atakaa katika mji huo, hadi hapo atakaposimama mbele ya mkutano kuhukumiwa, hadi kifo chake kuhani mkuu mwenye kuwapo siku hizo; ndipo yule mwuaji atarudi, na kuuendea mji wake mwenyewe, na nyumba yake mwenyewe, hadi mji huo alioutoka hapo alipokimbia.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo