Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Hesabu 35:22 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC

22 Lakini ikiwa alimsukuma ghafla pasipo kumchukia; au akamtupia kitu chochote pasipo kumvizia,

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

22 “Lakini kama mtu akimsukuma mwenzake kwa ghafla bila chuki au kumtupia kitu bila kumvizia

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

22 “Lakini kama mtu akimsukuma mwenzake kwa ghafla bila chuki au kumtupia kitu bila kumvizia

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

22 “Lakini kama mtu akimsukuma mwenzake kwa ghafla bila chuki au kumtupia kitu bila kumvizia

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

22 “ ‘Lakini kama mtu akimsukuma mwenziwe ghafula pasipo chuki, au kumtupia kitu pasipo kukusudia,

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

22 “ ‘Lakini kama mtu akimsukuma mwenziwe ghafula pasipo chuki, au kumtupia kitu pasipo kukusudia,

Tazama sura Nakili




Hesabu 35:22
8 Marejeleo ya Msalaba  

Lakini kama hakumvizia, ila Mungu amemtia mkononi mwake; basi nitakuonesha mahali atakapopakimbilia.


Ndipo mtajiwekea miji itakayokuwa ya makimbilio kwa ajili yenu; ili kwamba mwenye kumwua mtu, pasipo kukusudia kumwua, apate kukimbilia huko.


Tena kama alimsukuma kwa kumchukia au kama alimtupia kitu kwa kumvizia, hadi akafa;


au akampiga kwa mkono wake kwa kuwa ni adui, naye akafa; yeye aliyempiga lazima atauawa; yeye ni mwuaji; mwenye kutwaa kisasi cha damu atamwua mwuaji, hapo atakapokutana naye.


au kwa jiwe liwalo lote, ambalo kwa kupigwa kwalo humkini mtu kufa, bila kumwona akamtupia hata akafa, naye hakuwa adui yake, wala hakumtakia madhara;


kama aingiapo mtu na mwenziwe mwituni kwenda kukata kuni, akapeleka mkono wake na shoka ili kukata mti, likatoka shoka katika mpini, likampiga yule mwenziwe hata akafa; basi na akimbilie katika miji hii mmojawapo awe hai;


ili kwamba mwenye kuua mtu, aliyemwua mtu yeyote pasipo kukusudia, na pasipo kujua, apate kukimbilia huko; nayo itakuwa ni mahali pa kukimbilia kwenu, kumkimbia huyo ajilipizaye kisasi cha damu.


Na kama huyo mwenye kujilipiza kisasi cha damu akimfuatia, ndipo hawatamtoa huyo mwuaji kumtia mkononi mwake huyo; kwa sababu alimpiga mwenziwe naye hakujua, wala hakumchukia tangu hapo.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo