Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Hesabu 35:12 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC

12 Na hiyo miji itakuwa kwenu kuwa makimbilio, kumkimbia mwenye kulipiza kisasi, ili asiuawe mwenye kumwua mtu, hata atakaposimama mbele ya mkutano ahukumiwe.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

12 Miji hiyo itakuwa mahali pa kukimbilia usalama ili huyo mwuaji asiuawe na mwenye kulipiza kisasi kabla ya kuhukumiwa na jumuiya.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

12 Miji hiyo itakuwa mahali pa kukimbilia usalama ili huyo mwuaji asiuawe na mwenye kulipiza kisasi kabla ya kuhukumiwa na jumuiya.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

12 Miji hiyo itakuwa mahali pa kukimbilia usalama ili huyo mwuaji asiuawe na mwenye kulipiza kisasi kabla ya kuhukumiwa na jumuiya.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

12 Itakuwa mahali pa kukimbilia kutoka mlipiza kisasi, ili mtu aliyeshtakiwa kwa mauaji asife kabla ya kujitetea mbele ya mkutano.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

12 Itakuwa mahali pa kukimbilia kutoka mlipiza kisasi, ili kwamba mtu aliyeshtakiwa kwa mauaji asife kabla ya kujitetea mbele ya mkutano.

Tazama sura Nakili




Hesabu 35:12
10 Marejeleo ya Msalaba  

Na tazama, jamaa yote wameniinukia mimi mjakazi wako, wakasema, Mtoe yule aliyempiga nduguye, ili tupate kumwua yeye kwa maisha ya nduguye aliyemwua, hata na kumwua mrithi pia; ndivyo watakavyolizima kaa langu lililobaki, wasimwachie mume wangu jina wala mabaki usoni pa nchi.


Na hiyo miji mtakayowapa itakuwa kwenu ni miji sita ya kukimbilia.


Mwenye kutwaa kisasi cha damu ndiye atakayemwua mwuaji; hapo atakapokutana naye, atamwua.


Na hii ndiyo hukumu ya mwenye kuua mtu, atakayekimbilia huko awe hai; atakayemwua mwenziwe pasipo kukusudia, wala hakumchukia tangu hapo;


asije akaandamiwa mwuaji na mwenye kulipiza kisasi cha damu, moyo wake ukali na hasira, akampata kwa njia kuwa ndefu, akamwua; wala hana haki ya kuuawa, kwa kuwa hakumchukia tangu hapo.


Nena wewe na wana wa Israeli, uwaambie, Haya, toeni hiyo miji ya makimbilio, ambayo niliwaambia habari zake kwa mkono wa Musa;


Miji hiyo ndiyo miji iliyoamriwa kwa ajili ya wana wa Israeli wote, na kwa ajili ya mgeni akaaye kati yao ugenini, ili kwamba mtu yeyote atakayemwua mtu pasipo kukusudia apate kimbilia huko, asife kwa mkono wa mwenye kujilipiza kisasi cha damu, hadi hapo atakapokuwa amekwisha simama mbele ya mkutano.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo