Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -

Hesabu 31:47 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC

47 na katika hiyo nusu iliyokuwa ya wana wa Israeli, Musa akatwaa mmoja aliyetolewa katika kila hamsini, wa binadamu na wa wanyama, akawapa Walawi, wenye wajibu wa kuhudumu katika maskani ya BWANA; kama BWANA alivyomwagiza Musa.

Tazama sura Nakili

Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

47 Kutoka nusu hii waliyopewa Waisraeli, Mose alitwaa mmoja kati ya kila mateka hamsini na wanyama hamsini, kama alivyoamriwa na Mwenyezi-Mungu, akawapa Walawi ambao walihudumu katika hema la Mwenyezi-Mungu.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

47 Kutoka nusu hii waliyopewa Waisraeli, Mose alitwaa mmoja kati ya kila mateka hamsini na wanyama hamsini, kama alivyoamriwa na Mwenyezi-Mungu, akawapa Walawi ambao walihudumu katika hema la Mwenyezi-Mungu.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

47 Kutoka nusu hii waliyopewa Waisraeli, Mose alitwaa mmoja kati ya kila mateka hamsini na wanyama hamsini, kama alivyoamriwa na Mwenyezi-Mungu, akawapa Walawi ambao walihudumu katika hema la Mwenyezi-Mungu.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

47 Kutoka hiyo nusu iliyokuwa ya Waisraeli, Musa alichagua moja kati ya kila hamsini ya wanadamu na wanyama, kama Mwenyezi Mungu alivyomwagiza, naye aliwapa Walawi, ambao waliwajibika kutunza Maskani ya Mwenyezi Mungu.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

47 Kutoka hiyo nusu iliyokuwa ya Waisraeli, Musa alichagua moja kati ya kila hamsini ya wanadamu na wanyama, kama bwana alivyomwagiza, naye aliwapa Walawi, ambao waliwajibika kutunza Maskani ya bwana.

Tazama sura Nakili

Hesabu 31:47
12 Marejeleo ya Msalaba  

Njoni, enyi watumishi wote wa BWANA, Mhimidini BWANA Ninyi mnaohudumu usiku Katika nyumba ya BWANA.

Basi wana wa Israeli wakaenda na kufanya mambo hayo; vile vile kama BWANA alivyowaamuru Musa na Haruni, ndivyo walivyofanya.

Lakini Walawi watapanga hema zao kuizunguka maskani ya ushahidi pande zote, ili zisiwe hasira juu ya mkutano wa wana wa Israeli; kisha Walawi wahudumu katika hiyo Hema Takatifu.

Na katika hiyo nusu ya wana wa Israeli utatwaa mmoja atakayetolewa katika kila hamsini, katika wanadamu, na katika ng'ombe, na katika punda, na katika kondoo, maana, katika wanyama wote, ukawape Walawi, hao wenye wajibu wa kuhudumu maskani ya BWANA.

na wanadamu elfu kumi na sita;)

Na majemadari waliokuwa juu ya maelfu ya hilo jeshi, na viongozi wa maelfu, na viongozi wa mamia, wakamkaribia Musa;

Siku iyo hiyo Yoshua akawafanya kuwa ni wenye kupasua kuni, na wenye kuteka maji, kwa ajili ya mkutano, na kwa ajili ya madhabahu ya BWANA, hata siku hii ya leo, katika mahali hapo atakapopachagua.

Tufuate:

Matangazo

Matangazo