Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Hesabu 31:30 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC

30 Na katika hiyo nusu ya wana wa Israeli utatwaa mmoja atakayetolewa katika kila hamsini, katika wanadamu, na katika ng'ombe, na katika punda, na katika kondoo, maana, katika wanyama wote, ukawape Walawi, hao wenye wajibu wa kuhudumu maskani ya BWANA.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

30 Kutoka lile fungu la jumuiya nzima, chukua sehemu moja ya kila hamsini, iwe ni watu, ng'ombe, punda, kondoo na mbuzi. Hivyo utawapa Walawi ambao wana wajibu wa kuhudumu katika hema la Mwenyezi-Mungu.”

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

30 Kutoka lile fungu la jumuiya nzima, chukua sehemu moja ya kila hamsini, iwe ni watu, ng'ombe, punda, kondoo na mbuzi. Hivyo utawapa Walawi ambao wana wajibu wa kuhudumu katika hema la Mwenyezi-Mungu.”

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

30 Kutoka lile fungu la jumuiya nzima, chukua sehemu moja ya kila hamsini, iwe ni watu, ng'ombe, punda, kondoo na mbuzi. Hivyo utawapa Walawi ambao wana wajibu wa kuhudumu katika hema la Mwenyezi-Mungu.”

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

30 Kutoka fungu la Waisraeli, chukua kitu kimoja kati ya kila hamsini, ikiwa ni wanadamu, ng’ombe, punda, kondoo, mbuzi au wanyama wengine. Hivyo uwape Walawi, ambao wanawajibika kutunza Maskani ya Mwenyezi Mungu.”

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

30 Kutoka fungu la Waisraeli, chukua kitu kimoja kati ya kila hamsini, ikiwa ni wanadamu, ng’ombe, punda, kondoo, mbuzi au wanyama wengine. Hivyo uwape Walawi, ambao wanawajibika kutunza Maskani ya bwana.”

Tazama sura Nakili




Hesabu 31:30
21 Marejeleo ya Msalaba  

tena ni wajibu wao kuitunza hema ya kukutania na patakatifu na kuwasaidia wana wa Haruni, ndugu zao, katika utumishi wa nyumba ya BWANA.


Wakazipiga pia hema za ng'ombe, wakachukua kondoo wengi na ngamia, wakarudi Yerusalemu.


Lakini Walawi watapanga hema zao kuizunguka maskani ya ushahidi pande zote, ili zisiwe hasira juu ya mkutano wa wana wa Israeli; kisha Walawi wahudumu katika hiyo Hema Takatifu.


Na kazi ya Wageruhoni katika hema ya kukutania ni hiyo ya kuhudumu katika maskani, Hema na kifuniko chake, na pazia la mlango wa hema ya kukutania,


Na vitu watakavyovitunza ni hilo sanduku, na meza, na kinara cha taa, na madhabahu, na vile vyombo vya mahali patakatifu wavitumiavyo katika huduma yao, na pazia, na utumishi wake wote.


kisha uwatoze hao watu wa vita waliotoka kwenda vitani sehemu kwa ajili ya BWANA; mmoja katika mia tano, katika wanadamu, na katika ng'ombe, na katika punda, na katika kondoo;


twaa katika nusu yao, ukampe Eleazari kuhani, kuwa sadaka ya kuinuliwa kwa BWANA.


Musa na Eleazari kuhani wakafanya kama BWANA alivyomwagiza Musa.


lakini watawasaidia na ndugu zao katika hema ya kukutania, kufanya kazi zao, lakini wasitumike katika huo utumishi tena. Ndivyo utakavyowafanyia Walawi katika mambo ya ulinzi wao.


Jitunzeni nafsi zenu, na lile kundi lote nalo, ambalo Roho Mtakatifu amewaweka ninyi kuwa waangalizi ndani yake, mpate kulilisha kanisa lake Mungu, alilolinunua kwa damu yake mwenyewe.


Hapo tena inayohitajiwa katika mawakili, ndiyo mtu aonekane kuwa mwaminifu.


Mwambieni Arkipo, Iangalie sana huduma ile uliyopewa katika Bwana, ili uitimize.


Watiini viongozi wenu, na kuwanyenyekea; maana wao wanakesha kwa ajili ya roho zenu, kama watu watakaotoa hesabu, ili kwamba wafanye hivyo kwa furaha wala si kwa huzuni; maana haitawafaa ninyi.


Siku iyo hiyo Yoshua akawafanya kuwa ni wenye kupasua kuni, na wenye kuteka maji, kwa ajili ya mkutano, na kwa ajili ya madhabahu ya BWANA, hata siku hii ya leo, katika mahali hapo atakapopachagua.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo