Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Hesabu 31:13 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC

13 Basi Musa, na Eleazari kuhani, na wakuu wote wa huo mkutano, wakatoka nje kwenda kuwalaki nje ya kambi.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

13 Mose, kuhani Eleazari, na viongozi wote wa jumuiya ya Waisraeli walitoka kambini, wakaenda kuwalaki wanajeshi.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

13 Mose, kuhani Eleazari, na viongozi wote wa jumuiya ya Waisraeli walitoka kambini, wakaenda kuwalaki wanajeshi.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

13 Mose, kuhani Eleazari, na viongozi wote wa jumuiya ya Waisraeli walitoka kambini, wakaenda kuwalaki wanajeshi.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

13 Musa, kuhani Eleazari na viongozi wote wa jumuiya wakatoka kuwalaki nje ya kambi.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

13 Musa, kuhani Eleazari na viongozi wote wa jumuiya wakatoka kuwalaki nje ya kambi.

Tazama sura Nakili




Hesabu 31:13
9 Marejeleo ya Msalaba  

Abramu aliporudi kutoka kumpiga Kedorlaoma na wale wafalme waliokuwa pamoja naye, mfalme wa Sodoma akatoka amlaki katika bonde la Shawe, nalo ni Bonde la Mfalme.


Mtawala atakapofanya dhambi, na kutenda pasipo kukusudia neno lolote kati ya hayo ambayo BWANA, Mungu wake, aliyazuilia yasifanywe, naye amepata hatia;


Mtu agusaye maiti yeyote atakuwa najisi muda wa siku saba;


Nao wakawaleta mateka ya wanadamu, na mateka ya wanyama, na hizo nyara, na kuyaweka mbele ya Musa, na mbele ya Eleazari kuhani, na mbele ya mkutano wa wana wa Israeli, hapo kambini katika nchi tambarare za Moabu, zilizo karibu na Yordani hapo Yeriko.


Musa akawakasirikia majemadari wa jeshi, na hao makamanda wa maelfu, na makamanda wa mamia, hao waliorudi kutoka kupigana vita.


Waamrishe wana wa Israeli kwamba wamtoe kila mwenye ukoma kambini, na kila mtu aliye na kisonono, na kila aliye najisi kwa ajili ya maiti;


Samweli akaondoka asubuhi na mapema ili aonane na Sauli; Samweli akaambiwa ya kwamba, Sauli alifika Karmeli, na tazama, akajisimamishia mnara wa ukumbusho wake, akageuka, akapita, akateremkia Gilgali.


Kisha Daudi aliwafikia wale watu mia mbili, waliokuwa wametaka kuzimia, hata wasiweze kumfuata Daudi, wale waliowaacha wakae karibu na kijito cha Besori; nao wakatoka nje ili kumlaki Daudi, na kuwalaki hao watu waliokuwa pamoja naye, naye Daudi alipowakaribia hao watu, aliwasalimu.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo