Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Hesabu 29:17 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC

17 Tena siku ya pili mtasongeza ng'ombe dume wachanga kumi na wawili, na kondoo dume wawili, na wana-kondoo dume wa mwaka mmoja kumi na wanne wakamilifu;

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

17 “Siku ya pili mtatoa: Fahali wachanga kumi na wawili, kondoo madume wawili, wanakondoo wa kiume kumi na wanne, wa mwaka mmoja wasio na dosari.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

17 “Siku ya pili mtatoa: Fahali wachanga kumi na wawili, kondoo madume wawili, wanakondoo wa kiume kumi na wanne, wa mwaka mmoja wasio na dosari.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

17 “Siku ya pili mtatoa: fahali wachanga kumi na wawili, kondoo madume wawili, wanakondoo wa kiume kumi na wanne, wa mwaka mmoja wasio na dosari.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

17 “ ‘Katika siku ya pili, andaeni mafahali wachanga kumi na wawili, kondoo dume wawili, na wana-kondoo kumi na wanne wa mwaka mmoja, wote wasio na dosari.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

17 “ ‘Katika siku ya pili andaeni mafahali wachanga kumi na wawili, kondoo dume wawili, na wana-kondoo kumi na wanne wa mwaka mmoja, wote wasio na dosari.

Tazama sura Nakili




Hesabu 29:17
14 Marejeleo ya Msalaba  

Dhabihu na matoleo hukupendezwa nazo, Umetuzidishia ila masikio, Kafara na sadaka za dhambi hukuzitaka.


Nayo yatampendeza BWANA kuliko ng'ombe, Au ndama mwenye pembe na kwato.


Mwana-kondoo wenu atakuwa hana dosari, wa kiume wa mwaka mmoja; mtamtwaa katika kondoo au katika mbuzi.


Huu wingi wa sadaka zenu mnazonitolea una faida gani? Asema BWANA. Nimejaa mafuta ya kafara za kondoo dume, na mafuta ya wanyama walionona; nami siifurahii damu ya ng'ombe wala ya wana-kondoo wala ya mbuzi dume.


Maana nataka fadhili wala si sadaka; na kumjua Mungu kuliko sadaka za kuteketezwa.


Mtamsogezea BWANA sadaka kwa moto siku saba; siku ya nane kutakuwa na kusanyiko takatifu kwenu; nanyi mtamtolea BWANA sadaka kwa moto; ni mkutano wa makini huu; msifanye kazi yoyote ya utumishi.


nanyi mtasongeza sadaka ya kuteketezwa, sadaka isongezwayo kwa moto, harufu ya kupendeza kwa BWANA; ng'ombe dume wachanga kumi na watatu na kondoo dume wawili, na wana-kondoo dume wa mwaka mmoja kumi na wanne; wote watakuwa wakamilifu;


Basi, ndugu zangu, nawasihi, kwa huruma zake Mungu, itoeni miili yenu iwe dhabihu iliyo hai, takatifu, ya kumpendeza Mungu, ndiyo ibada yenu yenye maana.


Kwa kule kusema, Agano jipya, amelifanya lile la kwanza kuwa kuukuu. Lakini kitu kianzacho kuwa kikuukuu na kuchakaa kiko karibu kutoweka.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo