Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Hesabu 25:14 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC

14 Basi jina la Mwisraeli huyo aliyeuawa pamoja na yule mwanamke Mmidiani, aliitwa Zimri, mwana wa Salu, mkuu wa nyumba ya baba zake, katika kabila la Simeoni.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

14 Huyo Mwisraeli aliyeuawa pamoja na mwanamke wa Kimidiani aliitwa Zimri mwana wa Salu, kiongozi wa jamaa mojawapo katika kabila la Simeoni.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

14 Huyo Mwisraeli aliyeuawa pamoja na mwanamke wa Kimidiani aliitwa Zimri mwana wa Salu, kiongozi wa jamaa mojawapo katika kabila la Simeoni.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

14 Huyo Mwisraeli aliyeuawa pamoja na mwanamke wa Kimidiani aliitwa Zimri mwana wa Salu, kiongozi wa jamaa mojawapo katika kabila la Simeoni.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

14 Jina la Mwisraeli ambaye aliuawa pamoja na mwanamke Mmidiani ni Zimri mwana wa Salu, kiongozi wa jamaa ya Simeoni.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

14 Jina la Mwisraeli ambaye aliuawa pamoja na mwanamke wa Kimidiani ni Zimri mwana wa Salu, kiongozi wa jamaa ya Simeoni.

Tazama sura Nakili




Hesabu 25:14
10 Marejeleo ya Msalaba  

Wakapita wafanya biashara Wamidiani; basi wakamtoa Yusufu, wakampandisha kumtoa katika shimo, wakamuuza Yusufu kwa Waishmaeli kwa vipande vya fedha ishirini; nao wakamchukua Yusufu mpaka Misri.


Wakaondoka katika Midiani, wakafika Parani; wakachukua pamoja nao watu toka Parani, wakafika Misri, kwa Farao mfalme wa Misri; aliyempa nyumba, akaamuru apewe vyakula, akampa mashamba.


Wakuu wa makabila ya Israeli walikuwa hawa; wa Wareubeni, Eliezeri mwana wa Zikri; wa Wasimeoni, Shefatia mwana wa Maaka;


Basi sasa hofu ya BWANA na iwe juu yenu; aiweni waangalifu katika jambo mtendalo, kwa maana kwa BWANA, Mungu wetu hakuna upotoshaji wala kupendelea nafsi za watu au kupokea rushwa.


wale waliohesabiwa katika kabila la Simeoni, walikuwa watu elfu hamsini na tisa na mia tatu (59,300).


tena kwake yeye, na kizazi chake baada yake, litakuwa agano la ukuhani wa milele; kwa sababu alikuwa na wivu kwa ajili ya Mungu wake, na kuwafanyia upatanisho wana wa Israeli.


Na jina la huyo mwanamke Mmidiani aliyeuawa, aliitwa Kozbi, binti Suri; naye alikuwa kichwa cha watu wa nyumba ya baba zake huko Midiani.


Hawa ndizo jamaa wa Wasimeoni, watu elfu ishirini na mbili na mia mbili.


Wa kabila la Simeoni elfu kumi na mbili. Wa kabila la Lawi elfu kumi na mbili. Wa kabila la Isakari elfu kumi na mbili.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo