Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -




Hesabu 22:20 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC

20 Mungu akamjia Balaamu usiku, akamwambia, Kwa kuwa watu hawa wamekuja kukuita, nenda pamoja nao; lakini neno lile nitakalokuambia ndilo utakalolitenda, basi.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

20 Basi, Mungu akamjia Balaamu usiku huo, akamwambia, “Kama watu hawa wamekuja kukuita, nenda pamoja nao, lakini fanya tu kile nitakachokuambia.”

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

20 Basi, Mungu akamjia Balaamu usiku huo, akamwambia, “Kama watu hawa wamekuja kukuita, nenda pamoja nao, lakini fanya tu kile nitakachokuambia.”

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

20 Basi, Mungu akamjia Balaamu usiku huo, akamwambia, “Kama watu hawa wamekuja kukuita, nenda pamoja nao, lakini fanya tu kile nitakachokuambia.”

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

20 Usiku ule Mungu akamjia Balaamu na kumwambia, “Kwa kuwa watu hawa wamekuja kukuita wewe, nenda nao, lakini ufanye tu lile nitakalokuambia.”

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

20 Usiku ule bwana akamjia Balaamu na kumwambia, “Kwa kuwa watu hawa wamekuja kukuita wewe, nenda nao, lakini ufanye tu lile nitakalokuambia.”

Tazama sura Nakili




Hesabu 22:20
18 Marejeleo ya Msalaba  

Nikawaacha wakaenda kwa ukaidi wa mioyo yao, Waenende katika mashauri yao.


Kwa sababu ya kunighadhibikia kwako, na kwa sababu kutakabari kwako kumefika masikioni mwangu, nitatia kulabu yangu katika pua yako, na hatamu yangu midomoni mwako, nami nitakurudisha kwa njia ile ile uliyoijia.


Lakini BWANA akaniambia, Usiseme, Mimi ni mtoto; maana utakwenda kwa kila mtu nitakayekutuma kwake, nawe utasema kila neno nitakalokuamuru.


Nimekupa mfalme katika hasira yangu, nikamwondoa katika ghadhabu yangu.


Basi sasa nawasihi, kaeni hapa tena usiku huu, nipate kujua BWANA atakaloniambia zaidi.


Malaika wa BWANA akamwambia Balaamu Nenda pamoja na watu hawa, lakini neno lile nitakalokuambia, ndilo utakalosema. Basi Balaamu akaenda pamoja na wakuu wa Balaki.


Naye akajibu, akasema, Je! Hainipasi kuangalia, niseme neno lile BWANA atialo kinywani mwangu?


BWANA akaonana na Balaamu akatia neno kinywani mwake, akasema, Umrudie Balaki, ukaseme hivi.


Lakini Balaamu akajibu akamwambia Balaki, Je! Sikukuambia ya kwamba, Kila neno BWANA atakalolisema sina budi kulitenda?


BWANA akatia neno katika kinywa chake Balaamu, akasema, Umrudie Balaki; ukaseme maneno haya.


Hata Balaki angenipa nyumba yake imejaa fedha na dhahabu, siwezi kukiuka neno la BWANA, kutenda neno jema, wala neno baya, kwa nia yangu mwenyewe; BWANA atakalolinena ndilo nitakalolinena mimi.


Asema, yeye asikiaye maneno ya Mungu, Yeye aonaye maono ya Mwenyezi, Akianguka kifudifudi, amefumbuliwa macho;


Tufuate:

Matangazo


Matangazo