Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Hesabu 21:5 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC

5 Watu wakamnung'unikia Mungu, na Musa, Mbona mmetupandisha huku kutoka nchi ya Misri, ili tufe jangwani? Maana hapana chakula, wala hapana maji, na roho zetu zinakinai chakula hiki dhaifu.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

5 Basi, wakaanza kumnungunikia Mungu na Mose, wakisema, “Kwa nini mmetutoa Misri tuje tukafie humu jangwani? Humu hamna chakula wala maji; nasi tumechoshwa na chakula hiki duni.”

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

5 Basi, wakaanza kumnungunikia Mungu na Mose, wakisema, “Kwa nini mmetutoa Misri tuje tukafie humu jangwani? Humu hamna chakula wala maji; nasi tumechoshwa na chakula hiki duni.”

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

5 Basi, wakaanza kumnung'unikia Mungu na Mose, wakisema, “Kwa nini mmetutoa Misri tuje tukafie humu jangwani? Humu hamna chakula wala maji; nasi tumechoshwa na chakula hiki duni.”

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

5 wakamnung’unikia Mungu na Musa, wakisema, “Kwa nini umetupandisha kutoka Misri ili tufe jangwani? Hakuna mkate! Hakuna maji! Nasi tunachukia sana chakula hiki duni!”

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

5 wakamnung’unikia Mungu na Musa, wakisema, “Kwa nini umetupandisha kutoka Misri ili tufe jangwani? Hakuna mkate! Hakuna maji! Nasi tunachukia sana chakula hiki duni!”

Tazama sura Nakili




Hesabu 21:5
19 Marejeleo ya Msalaba  

Mungu huwapa wapweke makao yao; Huwapa wafungwa uhuru na kuwafanikisha; Bali wakaidi huishi katika nchi kavu.


Naam, walimwambia Mungu, wakasema, Je! Mungu aweza kuandaa meza jangwani?


Wakamwambia Musa, Je! Kwa sababu hapakuwa na makaburi katika Misri umetutoa huko ili tufe jangwani? Mbona umetutendea haya, kututoa katika nchi ya Misri?


Ndipo watu wakamnung'unikia Musa, wakisema, Tunywe nini?


Wana wa Israeli walipokiona, wakaambiana, Nini hiki? Maana hawakujua ni kitu gani. Musa akawaambia, Ndio mkate ambao BWANA amewapa ninyi, mle.


Na nyumba ya Israeli wakakiita jina lake Mana; nacho kilikuwa mfano wa chembe za mtama, nyeupe; na utamu wake ulikuwa kama utamu wa maandazi membamba yaliyoandaliwa kwa asali.


Nafsi iliyoshiba hukinai sega la asali; Bali nafsi yenye njaa huona kila kitu kichungu kuwa kitamu.


Lakini watoto hao waliniasi; hawakuenda katika amri zangu, wala hawakuzishika hukumu zangu kuzitenda, ambazo mwanadamu ataishi kwazo kama akizitenda; walizitia unajisi sabato zangu, ndipo nikasema, kwamba nitamwaga ghadhabu yangu juu yao, ili kuitimiza hasira yangu juu yao jangwani.


lakini mtakula muda wa mwezi mzima, hadi hapo nyama hiyo itakapotoka katika mianzi ya pua zenu, nanyi mtaikinai, kwa sababu mmemkataa BWANA aliye kati yenu, na kulia mbele zake, mkisema, Tulitoka Misri kwa maana gani?


Lakini siku ya pili yake mkutano wote wa wana wa Israeli wakamnung'unikia Musa, na Haruni, wakasema, Ninyi mmewaua watu wa BWANA.


Kisha wana wa Israeli wakanena na Musa, na kumwambia, Angalia, sisi tunakufa, tunaangamia, sote tunaangamia.


Wala tusimjaribu Bwana, kama wengine wao walivyomjaribu, wakauawa na nyoka.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo