Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Hesabu 21:2 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC

2 Basi Israeli akaweka nadhiri kwa BWANA akasema, Kama wewe utawatia watu hawa mikononi mwangu kweli ndipo mimi nitaiharibu miji yao kabisa.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

2 Hapo, Waisraeli wakamwekea Mwenyezi-Mungu nadhiri wakisema: “Kama utawatia watu hawa mikononi mwetu, basi tutaiangamiza kabisa miji yao.”

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

2 Hapo, Waisraeli wakamwekea Mwenyezi-Mungu nadhiri wakisema: “Kama utawatia watu hawa mikononi mwetu, basi tutaiangamiza kabisa miji yao.”

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

2 Hapo, Waisraeli wakamwekea Mwenyezi-Mungu nadhiri wakisema: “Kama utawatia watu hawa mikononi mwetu, basi tutaiangamiza kabisa miji yao.”

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

2 Ndipo Israeli akaweka nadhiri hii kwa Mwenyezi Mungu: “Ikiwa utawatia watu hawa mikononi mwetu, tutaiangamiza kabisa miji yao.”

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

2 Ndipo Israeli akaweka nadhiri hii kwa bwana: “Ikiwa utawatia watu hawa mikononi mwetu, tutaiangamiza kabisa miji yao.”

Tazama sura Nakili




Hesabu 21:2
15 Marejeleo ya Msalaba  

Yakobo akaweka nadhiri akisema, Mungu akiwa pamoja nami, akinilinda katika njia niiendeayo, na kunipa chakula nile, na nguo nivae;


Nitaziondoa nadhiri zangu kwa BWANA, Naam, mbele ya watu wake wote.


Vile alivyomwapia BWANA, Akaweka nadhiri kwa ewe Mwenye nguvu wa Yakobo.


Mtu awaye yote asiyempenda Bwana, na awe amelaaniwa. Maranatha.


hakika yako uwapige wenyeji wa mji ule kwa makali ya upanga, kwa kuwaangamiza kabisa, pamoja na vitu vyote vilivyomo, na wanyama walio humo, kwa makali ya upanga.


Na nyara zake zote uzikusanyie katikati ya njia yake; na mji uuteketeze kwa moto, na nyara zake zote, kuwe sadaka kamili ya kuteketezwa kwa BWANA, Mungu wako; nao utakuwa magofu milele; usijengwe tena.


Lakini katika miji ya mataifa haya akupayo BWANA, Mungu wako, kuwa urithi, usihifadhi kuwa hai kitu chochote kipumzikacho;


wakati BWANA, Mungu wako, atakapowatoa mbele yako, nawe utawapiga; wakati huo ndipo uwaondoe kabisa; usifanye agano nao, wala kuwahurumia; wala usioane nao;


Na mji huu utakuwa wakfu kwa BWANA, mji wenyewe na vitu vyote vilivyomo; isipokuwa Rahabu, yule kahaba, ataishi, yeye na watu wote walio pamoja naye nyumbani, kwa sababu aliwaficha hao wapelelezi tuliowatuma.


Naye Yoshua akawaapisha kiapo wakati ule, akasema, Na alaaniwe na BWANA mtu yule atakayeinuka na kutaka kuujenga tena mji huu wa Yeriko; atakayeweka msingi wake mzaliwa wake wa kwanza na afe. Tena atakayesimamisha malango yake mtoto wake wa kiume aliye mdogo na afe.


Naye Yeftha akamwekea BWANA nadhiri, akasema, Ikiwa utawatia wana wa Amoni mkononi mwangu kweli,


Akaweka nadhiri, akasema, Ee BWANA wa majeshi, ikiwa wewe utayaangalia mateso la mjakazi wako, na kunikumbuka, wala usinisahau mimi mjakazi wako, na kunipa mimi mjakazi wako mtoto wa kiume, ndipo mimi nitakapompa BWANA huyo mtoto siku zote za maisha yake, wala wembe hautamfikia kichwani kamwe.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo