Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Hesabu 18:24 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC

24 Kwa kuwa zaka ya wana wa Israeli, waisongezayo kuwa sadaka ya kuinuliwa kwa BWANA, nimewapa Walawi kuwa urithi wao; kwa hiyo nimewaambia, ya kwamba, katika wana wa Israeli hawatakuwa na urithi wowote.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

24 kwa sababu zaka wanazonitolea Waisraeli nimewapa kuwa urithi wao. Ndio maana nimesema kwamba wao hawatakuwa na urithi kati ya Waisraeli.”

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

24 kwa sababu zaka wanazonitolea Waisraeli nimewapa kuwa urithi wao. Ndio maana nimesema kwamba wao hawatakuwa na urithi kati ya Waisraeli.”

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

24 kwa sababu zaka wanazonitolea Waisraeli nimewapa kuwa urithi wao. Ndio maana nimesema kwamba wao hawatakuwa na urithi kati ya Waisraeli.”

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

24 Badala yake, ninawapa Walawi zaka zote zinazotolewa na Waisraeli kama sadaka kwa Mwenyezi Mungu kuwa urithi wao. Hiyo ndiyo sababu nimesema hivi kuwahusu: ‘Hawatakuwa na urithi miongoni mwa Waisraeli.’ ”

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

24 Badala yake, ninawapa Walawi zaka zote zinazotolewa na Waisraeli kama sadaka kwa bwana kuwa urithi wao. Hiyo ndiyo sababu nimesema hivi kuhusu wao: ‘Hawatakuwa na urithi miongoni mwa Waisraeli.’ ”

Tazama sura Nakili




Hesabu 18:24
10 Marejeleo ya Msalaba  

Naye kuhani, mwana wa Haruni, atakuwako pamoja na Walawi, watwaapo zaka Walawi; nao Walawi wataipandisha zaka ya hizo zaka nyumbani kwa Mungu wetu, vyumbani, katika nyumba ya hazina.


Ndipo Yuda wote walipoleta zaka za nafaka, na mvinyo, na mafuta, kwenye hazina.


Tena zaka yote ya nchi, kama ni mbegu ya nchi, au kama ni matunda ya nchi, ni ya BWANA; ni takatifu kwa BWANA.


Kisha BWANA akanena na Musa, na kumwambia,


Tena utanena na Walawi, na kuwaambia, Hapo mtakapoitwaa zaka mkononi mwa wana wa Israeli niliyowapa ninyi kutoka kwao kuwa urithi wenu, ndipo mtakaposongeza sadaka ya kuinuliwa kwa BWANA katika hiyo, iwe zaka katika hiyo zaka.


Na hao waliohesabiwa kwao walikuwa elfu ishirini na tatu, kila mwanamume tangu huyo aliyepata umri wa mwezi mmoja, na zaidi; kwa kuwa hawakuhesabiwa katika wana wa Israeli, kwa sababu hawakupewa urithi katika wana wa Israeli.


Ndipo asiwe na fungu Lawi, wala urithi pamoja na nduguze; BWANA ndiye urithi wake, kwa mfano wa vile alivyomwambia BWANA, Mungu wako.)


Utakapokwisha kutoa zaka, katika zaka zote za mavuno yako mwaka wa tatu, ambao ndio mwaka wa kutolea zaka, umpe zile zaka Mlawi, na mgeni, na yatima, na mjane, wapate kula ndani ya malango yako na kushiba;


Lakini hakuwapa watu wa kabila la Lawi urithi wowote ule; maana sadaka za BWANA, Mungu wa Israeli, zisongezwazo kwa njia ya moto ndizo urithi wake huyo, kama alivyomwambia.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo