Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -




Hesabu 15:36 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC

36 Basi mkutano wote wakampeleka nje ya kambi, nao wakampiga kwa mawe, akafa; kama BWANA alivyomwagiza Musa.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

36 Basi, watu wakamtoa nje ya kambi, wakampiga mawe mpaka akafa, kama Mwenyezi-Mungu alivyomwamuru Mose.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

36 Basi, watu wakamtoa nje ya kambi, wakampiga mawe mpaka akafa, kama Mwenyezi-Mungu alivyomwamuru Mose.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

36 Basi, watu wakamtoa nje ya kambi, wakampiga mawe mpaka akafa, kama Mwenyezi-Mungu alivyomwamuru Mose.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

36 Hivyo kusanyiko wakamtoa nje ya kambi na kumpiga mawe hadi akafa, kama Mwenyezi Mungu alivyomwamuru Musa.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

36 Hivyo kusanyiko likamtoa nje ya kambi na kumpiga mawe hadi akafa, kama bwana alivyomwamuru Musa.

Tazama sura Nakili




Hesabu 15:36
6 Marejeleo ya Msalaba  

Na hao watu wawili, watu wasiofaa, wakaingia, wakaketi mbele yake; wale watu wasiofaa wakamshuhudia Nabothi mbele ya watu, wakasema, Nabothi amemtukana Mungu na mfalme. Ndipo wakamchukua nje ya mji, wakampiga kwa mawe hata akafa.


Tena uwaambie wana wa Israeli, Mtu yeyote miongoni mwa wana wa Israeli, au miongoni mwa wageni waishio katika Israeli, atakayetoa katika kizazi chake na kumpa Moleki, sharti atauawa; wenyeji wa nchi watampiga kwa mawe.


BWANA akamwambia Musa, Mtu huyo lazima atauawa; mkutano wote watampiga kwa mawe huko nje ya kambi.


Kisha BWANA akasema na Musa, na kumwambia,


Wanaume wote wa mji wake na wamtupie mawe, afe; ndivyo utakavyoondoa uovu katikati yako; na Israeli wote watasikia na kuogopa.


Yoshua akasema, Mbona umetufadhaisha hivi? BWANA atakufadhaisha wewe leo. Ndipo Israeli wote wakampiga kwa mawe, kisha wakawateketeza kwa moto, na kuwapiga kwa mawe.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo