Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Hesabu 15:30 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC

30 Lakini mtu afanyaye neno lolote kwa kusudi, kama ni mzalia, kama ni mgeni, huyo amtukana BWANA; na mtu huyo atatupiliwa mbali na watu wake.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

30 “Lakini mtu yeyote atakayekosa kwa makusudi, awe mwananchi au mgeni, atakuwa anamdhihaki Mwenyezi-Mungu, na ni lazima akatiliwe mbali miongoni mwa watu wake.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

30 “Lakini mtu yeyote atakayekosa kwa makusudi, awe mwananchi au mgeni, atakuwa anamdhihaki Mwenyezi-Mungu, na ni lazima akatiliwe mbali miongoni mwa watu wake.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

30 “Lakini mtu yeyote atakayekosa kwa makusudi, awe mwananchi au mgeni, atakuwa anamdhihaki Mwenyezi-Mungu, na ni lazima akatiliwe mbali miongoni mwa watu wake.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

30 “ ‘Lakini yeyote ambaye amefanya dhambi kwa dharau awe mzawa au mgeni, anamkufuru Mwenyezi Mungu, naye mtu huyo ni lazima akatiliwe mbali na watu wake.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

30 “ ‘Lakini yeyote ambaye amefanya dhambi kwa dharau awe mzawa au mgeni, anamkufuru bwana, naye mtu huyo ni lazima akatiliwe mbali na watu wake.

Tazama sura Nakili




Hesabu 15:30
30 Marejeleo ya Msalaba  

Na mwanamume mwenye govi asiyetahiriwa nyama ya govi lake, mtu yule atatengwa na watu wake; amelivunja agano langu.


Na waovu nuru yao huzuiliwa isiwafikie, Na mkono ulioinuka huvunjika.


Umzuie mtumishi wako asitende mambo ya kiburi, Yasinitawale mimi. Ndipo nitakapokuwa kamili, Nami nitakuwa safi, sina kosa lililo kubwa.


Maana mvuto wa nyumba yako umenila, Na laumu zao wanaokulaumu zimenipata.


Ee BWANA, uyakumbuke hayo, adui amelaumu, Na watu wapumbavu wamelidharau jina lako.


Ee Mungu, usimame, ujitetee mwenyewe, Ukumbuke unavyotukanwa na mpumbavu mchana kutwa.


Uwalipe jirani zetu mara saba vifuani mwao Laumu zao walizokulaumu, Ee Bwana.


Ambayo adui zako wamesimanga, Ee BWANA, Naam, wamezisimanga hatua za masihi wako.


Lakini, mtu akimwendea mwenziwe kwa kujikinai, kusudi apate kumwua kwa hila; huyo utamwondoa hata madhabahuni pangu, auawe.


Mtu yeyote atakayechanganya mafuta mfano wa haya, au mtu yeyote atakayetia mafuta haya juu ya mgeni, mtu huyo atatengwa mbali na watu wake.


Amwoneaye maskini humsuta Muumba wake; Bali yeye awahurumiaye wahitaji humheshimu.


Basi, mwanadamu, sema na nyumba ya Israeli, uwaambie, Bwana MUNGU asema hivi; Baba zenu wamenitukana kwa jambo hili, kwa kuwa wametenda kosa juu yangu.


Na mtu aziniye na mke wa mtu mwingine, yeye aziniye na mke wa jirani yake, mwanamume aziniye, na mwanamke aziniye, hakika watauawa.


Mimi nami nitamkazia uso wangu mtu huyo, na nitamtenga na watu wake; kwa kuwa ametoa katika kizazi chake na kumpa Moleki, ili kupatia unajisi patakatifu pangu, na kulinajisi jina langu takatifu.


Na mtu yule atakayewaendea wenye pepo, na wachawi, ili kuzini pamoja nao, nitakaza uso wangu juu ya mtu yule, nitamtenga na watu wake.


Mtakuwa na sheria moja kwa huyo afanyaye neno lolote pasipo kujua, kwa huyo aliyezaliwa kwenu kati ya wana wa Israeli, na kwa mgeni akaaye kati yao.


Lakini mtu aliye safi, wala hakuwa katika safari, naye amekosa kuishika Pasaka, mtu huyo atatengwa na watu wake; kwa sababu hakumtolea BWANA matoleo kwa wakati wake ulioamriwa, mtu huyo atachukua dhambi yake.


Naye mtu yeyote atakayenena neno juu ya Mwana wa Adamu atasamehewa, bali yeye atakayenena neno juu ya Roho Mtakatifu hatasamehewa katika ulimwengu wa sasa, wala katika ule ujao.


Hata ingawa niliwaambia, hamkunisikiza, bali mliasi amri ya Bwana, makajiamini na kulewa mlimani.


Isipokuwa niliogopa makamio ya adui, Adui zao wasije wakafikiri uongo, Wasije wakasema, Mkono wetu umetukuka, Wala BWANA hakuyafanya haya yote.


Maana, kama tukifanya dhambi kusudi baada ya kuupokea ujuzi wa ile kweli, haibaki tena dhabihu kwa ajili ya dhambi;


Mwaonaje? Haikumpasa adhabu iliyo kubwa zaidi mtu yule aliyemkanyaga Mwana wa Mungu, na kuihesabu damu ya agano aliyotakaswa kwayo kuwa ni kitu ovyo, na kumfanyia jeuri Roho wa neema?


na hasa wale waufuatao mwili katika tamaa ya mambo machafu, na kudharau mamlaka.


Mtu akimwona ndugu yake anatenda dhambi isiyo ya mauti, ataomba, na Mungu atampa uzima kwa ajili ya hao watendao dhambi isiyo ya mauti. Iko dhambi iliyo ya mauti. Sisemi ya kwamba ataomba kwa ajili ya hiyo.


Mtu mmoja akimkosea mwenzake, Mungu atamhukumu; lakini mtu akimkosea BWANA, ni nani atakayemtetea? Lakini hawakuisikia sauti ya baba yao, kwa sababu BWANA amekusudia kuwaua.


Na kwa hiyo nimeapa juu ya nyumba ya Eli, ya kwamba uovu wa nyumba ya Eli hautasafika kwa dhabihu wala kwa sadaka hata milele.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo