Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Hesabu 14:37 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC

37 watu hao walioileta habari mbaya ya nchi wakafa kwa tauni mbele ya BWANA.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

37 watu hao waliotoa taarifa ya uovu kuhusu hiyo nchi, walikufa kwa pigo mbele ya Mwenyezi-Mungu.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

37 watu hao waliotoa taarifa ya uovu kuhusu hiyo nchi, walikufa kwa pigo mbele ya Mwenyezi-Mungu.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

37 watu hao waliotoa taarifa ya uovu kuhusu hiyo nchi, walikufa kwa pigo mbele ya Mwenyezi-Mungu.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

37 watu hawa waliohusika kueneza taarifa mbaya kuhusu hiyo nchi walipigwa na kuanguka kwa tauni mbele za Mwenyezi Mungu.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

37 watu hawa waliohusika kueneza taarifa mbaya kuhusu hiyo nchi walipigwa na kuanguka kwa tauni mbele za bwana.

Tazama sura Nakili




Hesabu 14:37
17 Marejeleo ya Msalaba  

Hata watu elfu wakianguka ubavuni pako. Naam, watu elfu kumi katika mkono wako wa kulia! Wewe hutakaribiwa na maafa.


basi, BWANA asema hivi, Tazama, nitamwadhibu Shemaya, Mnehelami, na wazawa wake; hatakuwa na mtu atakayekaa katika watu hawa, wala hatayaona mema nitakayowatendea watu wangu, asema BWANA; kwa sababu amenena maneno ya uasi juu ya BWANA.


Kisha moto ukatoka hapo mbele za BWANA, na ukawateketeza, nao wakafa mbele za BWANA.


Wakawaletea wana wa Israeli habari mbaya ya ile nchi waliyoipeleleza, wakasema, Ile nchi tuliyopita kati yake ili kuipeleleza, ni nchi inayowala wakazi wake; na watu wote tuliowaona ndani yake ni watu wakubwa mno.


Nitawapiga kwa tauni, na kuwaondolea urithi wao, nami nitakufanya wewe kuwa taifa kubwa, kisha yenye nguvu kuliko wao.


Lakini Yoshua mwana wa Nuni, na Kalebu mwana wa Yefune, wakabaki hai miongoni mwa wale watu waliokwenda kuipeleleza nchi.


Kisha moto ukatoka kwa BWANA, ukawateketeza hao watu mia mbili hamsini waliofukiza uvumba.


Basi waliokufa kwa tauni walikuwa elfu kumi na nne na mia saba, zaidi ya hao waliokufa katika jambo la Kora.


Watu wakashindana na Musa, wakanena, wakisema, Ingekuwa heri kama tungekufa wakati ule ndugu zetu walipokufa mbele za BWANA!


punda akaniona, akageuka upande mbele zangu mara tatu hizi; kama asingejiepusha nami, bila shaka ningalikuua wewe, nikamwacha yeye hai.


Nao waliokufa kwa pigo hilo idadi yao ilikuwa elfu ishirini na nne.


Wala msinung'unike, kama wengine wao walivyonung'unika, wakauawa na mharibifu.


Lakini wengi sana katika wao, Mungu hakupendezwa nao; maana waliangamizwa jangwani.


Tena ni akina nani aliochukizwa nao miaka arubaini? Si wale waliokosa, ambao mizoga yao ilianguka katika jangwa?


Tena ni akina nani aliowaapia ya kwamba hawataingia katika pumziko lake, ila wale walioasi?


Tena napenda kuwakumbusha, ijapokuwa mmekwisha kujua haya yote, ya kwamba Bwana, akiisha kuwaokoa watu katika nchi ya Misri, aliwaangamiza baadaye wale wasioamini.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo