Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Hesabu 14:28 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC

28 Waambieni, Kama niishivyo, asema BWANA, hakika yangu kama ninyi mlivyonena masikioni mwangu, ndivyo nitakavyowafanyia ninyi;

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

28 Sasa wajibu hivi: Kama niishivyo, nasema mimi Mwenyezi-Mungu, nitawatendeeni yaleyale niliyosikia mkiyasema:

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

28 Sasa wajibu hivi: Kama niishivyo, nasema mimi Mwenyezi-Mungu, nitawatendeeni yaleyale niliyosikia mkiyasema:

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

28 Sasa wajibu hivi: Kama niishivyo, nasema mimi Mwenyezi-Mungu, nitawatendeeni yaleyale niliyosikia mkiyasema:

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

28 Hivyo waambie, ‘Hakika kama niishivyo, asema Mwenyezi Mungu, nitawafanyia vitu vilevile nilivyosikia mkisema:

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

28 Hivyo waambie, ‘Hakika kama niishivyo, asema bwana, nitawafanyia vitu vilevile nilivyosikia mkisema:

Tazama sura Nakili




Hesabu 14:28
18 Marejeleo ya Msalaba  

Macho yake mwenyewe na yaone uharibifu wake, Akanywe ghadhabu zake Mwenyezi.


Ndipo alipowainulia mkono wake na kuwaapia, Ya kuwa atawaangamiza jangwani,


Ndipo Nikaapa kwa hasira yangu Hawataingia katika pumziko langu.


Maana mimi ni BWANA; mimi nitanena, na neno lile nitakalolinena litatimizwa; wala halitakawilishwa tena; maana katika siku zenu, Ewe nyumba iliyoasi, nitalinena neno hilo na kulitimiza, asema Bwana MUNGU.


Kisha hao watu walikuwa kama wanung'unikao, wakinena maovu masikioni mwa BWANA; BWANA aliposikia hayo, hasira zake zikawaka; na moto wa BWANA ukawaka kati yao, ukateketeza hadi viunga vya kambi.


Kisha wana wa Israeli wote wakamnung'unikia Musa na Haruni; mkutano wote wakawaambia, Ingekuwa heri kama tungalikufa katika nchi ya Misri, au, ingekuwa heri kama tungalikufa katika jangwa hili.


lakini hakika yangu, kama niishivyo, tena kama dunia hii nzima itakavyojawa na utukufu wa BWANA;


hakika yangu hawataiona hiyo nchi niliyowaapia baba zao, wala katika hao wote walionidharau hapana atakayeiona;


Kisha Musa akawaambia wana wa Israeli wote maneno haya, na hao watu wakaomboleza sana.


Hakika yangu hapana mtu mmoja katika wale watu waliotoka Misri, tangu huyo aliyepata umri wa miaka ishirini, na zaidi, atakayeiona hiyo nchi niliyomwapia Abrahamu, na Isaka, na Yakobo; kwa sababu hawakuniandama kwa moyo wote;


BWANA akaisikia sauti ya maneno yenu, akaghadhibika, akaapa, akasema,


Hakika yangu hapana mmoja miongoni mwa watu hawa wa kizazi hiki kibaya atakayeiona nchi hiyo nzuri, niliyowaapia baba zenu kuwapa,


Na siku tulizokuwa tukienda kutoka Kadesh-barnea hata tulipovuka kijito cha Zeredi, ilikuwa ni miaka thelathini na minane; maana, hata walipokwisha kuangamizwa watu wa vita kutoka kati ya kambi, kizazi chao chote, kama walivyoapiwa na BWANA.


Tena mkono wa BWANA ulikuwa juu yao ili kuwaangamiza, kuwatoa katika kambi hadi walipouwawa.


Maana, nainua mkono wangu mbinguni, Na kusema, Kama Mimi niishivyo milele,


Tena ni akina nani aliochukizwa nao miaka arubaini? Si wale waliokosa, ambao mizoga yao ilianguka katika jangwa?


Tufuate:

Matangazo


Matangazo