Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Hesabu 14:13 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC

13 Basi Musa akamwambia BWANA, Ndipo Wamisri watasikia habari hiyo; kwa kuwa wewe uliwaleta watu hawa kwa uweza wako, kutoka kati yao;

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

13 Lakini Mose akamwambia Mwenyezi-Mungu, “Uliwatoa watu hawa nchini Misri kwa nguvu yako. Wamisri watakaposikia kwamba umewatenda hivyo watu wako,

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

13 Lakini Mose akamwambia Mwenyezi-Mungu, “Uliwatoa watu hawa nchini Misri kwa nguvu yako. Wamisri watakaposikia kwamba umewatenda hivyo watu wako,

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

13 Lakini Mose akamwambia Mwenyezi-Mungu, “Uliwatoa watu hawa nchini Misri kwa nguvu yako. Wamisri watakaposikia kwamba umewatenda hivyo watu wako,

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

13 Musa akamwambia Mwenyezi Mungu, “Ndipo Wamisri watasikia juu ya jambo hili! Kwa uweza wako uliwapandisha watu hawa kutoka miongoni mwao.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

13 Musa akamwambia bwana, “Ndipo Wamisri watasikia juu ya jambo hili! Kwa uweza wako uliwapandisha watu hawa kutoka miongoni mwao.

Tazama sura Nakili




Hesabu 14:13
9 Marejeleo ya Msalaba  

Akasema ya kuwa atawaangamiza Kama Musa, mteule wake, asingalisimama, Mbele zake na kusimama palipobomoka, Ili aigeuze hasira yake asije akawaangamiza.


Ndipo BWANA akaniambia, Hata wangesimama mbele zangu Musa na Samweli, moyo wangu usingewaelekea watu hawa; watupe, watoke mbele za macho yangu, wakaende zao.


Lakini nilitenda kwa ajili ya jina langu, lisitiwe unajisi machoni pa mataifa, ambao niliwatoa mbele ya macho yao.


Lakini nilitenda kwa ajili ya jina langu, ili lisitiwe unajisi mbele ya macho ya mataifa, ambao walikaa pamoja nao, ambao machoni pao nilijidhihirisha kwao, kwa kuwatoa katika nchi ya Misri.


Isipokuwa niliogopa makamio ya adui, Adui zao wasije wakafikiri uongo, Wasije wakasema, Mkono wetu umetukuka, Wala BWANA hakuyafanya haya yote.


visivyoweza kusaidia wala kuokoa, kwa kuwa havifai kitu. Maana BWANA hatawaacha watu wake kwa ajili ya jina lake kuu; kwa kuwa imempendeza BWANA kuwafanya ninyi kuwa watu wake mwenyewe.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo