Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -

Hesabu 11:31 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC

31 Kisha upepo ukavuma kutoka kwa BWANA, nao ukaleta kware kutoka pande za baharini, nao ukawaacha wakaanguka karibu na kambi, kama kiasi cha mwendo wa siku moja upande huu, na kama kiasi cha mwendo wa siku moja upande ule, kuizunguka, nao wakafikia kiasi cha dhiraa mbili juu ya uso wa nchi.

Tazama sura Nakili

Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

31 Baadaye Mwenyezi-Mungu akavumisha upepo kwa ghafla, ukaleta kware kutoka baharini na kuwafanya watue kando ya kambi, mwendo wa siku moja hivi kila upande kuizunguka kambi, wakarundikana chini karibu kimo cha mita moja hivi.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

31 Baadaye Mwenyezi-Mungu akavumisha upepo kwa ghafla, ukaleta kware kutoka baharini na kuwafanya watue kando ya kambi, mwendo wa siku moja hivi kila upande kuizunguka kambi, wakarundikana chini karibu kimo cha mita moja hivi.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

31 Baadaye Mwenyezi-Mungu akavumisha upepo kwa ghafla, ukaleta kware kutoka baharini na kuwafanya watue kando ya kambi, mwendo wa siku moja hivi kila upande kuizunguka kambi, wakarundikana chini karibu kimo cha mita moja hivi.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

31 Kisha ukatokea upepo kutoka kwa Mwenyezi Mungu, nao ukawaletea kware kutoka baharini. Ukawaangusha kwenye eneo lote linalozunguka kambi na kujaa ardhini kimo cha mita moja hivi kutoka ardhini kwenye eneo la umbali wa mwendo wa siku moja kila upande.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

31 Kisha ukatokea upepo kutoka kwa bwana, nao ukawaletea kware kutoka baharini. Ukawaangusha kwenye eneo lote linalozunguka kambi na kujaa ardhini kimo cha mita moja hivi kutoka ardhini kwenye eneo la umbali wa mwendo wa siku moja kila upande.

Tazama sura Nakili

Hesabu 11:31
9 Marejeleo ya Msalaba  

Walimwomba naye akaleta kware, Na kuwashibisha chakula cha mbinguni.

Akawapa walichomwomba, Lakini akawatumia ugonjwa wa kuwakondesha.

Ndiye apandishaye mvuke toka miisho ya nchi; Huifanyia mvua umeme; Hutoa upepo katika ghala zake.

Basi Musa akainyosha fimbo yake juu ya nchi ya Misri, na BWANA akaleta upepo kutoka mashariki juu ya nchi, mchana kutwa, na usiku kucha; kulipopambazuka ule upepo wa mashariki ukawaleta nzige.

BWANA akaugeuza upepo wa magharibi wenye nguvu nyingi, ambao uliwaondoa wale nzige na kuwapeleka katika Bahari ya Shamu; hakusalia hata nzige mmoja ndani ya mipaka yote ya Misri.

Ulivuma kwa upepo wako, bahari ikawafunikiza; Wakazama kama risasi ndani ya maji makuu.

Ikawa wakati wa jioni, kware wakaja, wakaifunikiza kambi; na wakati wa asubuhi umande ulikuwa juu ya nchi pande zote za kituo.

Kisha Musa akaenda akaingia kambini, yeye na wale wazee wa Israeli.

Tufuate:

Matangazo

Matangazo