Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -




Hesabu 11:29 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC

29 Musa akamwambia, Je! Umekuwa na wivu kwa ajili yangu; ingekuwa heri kama watu wote wa BWANA wangekuwa manabii na kama BWANA angewatia roho yake.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

29 Lakini Mose akamjibu, “Je, unaona wivu kwa ajili yangu? Laiti Mwenyezi-Mungu angewapa watu wake wote roho yake nao wakawa manabii!”

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

29 Lakini Mose akamjibu, “Je, unaona wivu kwa ajili yangu? Laiti Mwenyezi-Mungu angewapa watu wake wote roho yake nao wakawa manabii!”

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

29 Lakini Mose akamjibu, “Je, unaona wivu kwa ajili yangu? Laiti Mwenyezi-Mungu angewapa watu wake wote roho yake nao wakawa manabii!”

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

29 Lakini Musa akajibu, “Je, unaona wivu kwa ajili yangu? Ningetamani watu wote wa Mwenyezi Mungu wangekuwa manabii na kwamba Mwenyezi Mungu angeweka Roho yake juu yao!”

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

29 Lakini Musa akajibu, “Je, unaona wivu kwa ajili yangu? Ningetamani watu wote wa bwana wangekuwa manabii na kwamba bwana angeweka Roho yake juu yao!”

Tazama sura Nakili




Hesabu 11:29
17 Marejeleo ya Msalaba  

Nanyi mtajua ya kuwa mimi ni katikati ya Israeli, na ya kuwa mimi ndimi BWANA, Mungu wenu, wala hakuna mwingine; na watu wangu hawatatahayari kamwe.


Kwa maana, angalieni, siku zile, na wakati ule, nitakapowarudisha mateka wa Yuda na Yerusalemu,


Kisha Musa akaenda akaingia kambini, yeye na wale wazee wa Israeli.


Akawaambia, Mavuno ni mengi, lakini wafanya kazi ni wachache; basi mwombeni Bwana wa mavuno apeleke wafanya kazi katika mavuno yake.


Paulo akamjibu, Namwomba Mungu kwamba, ikiwa kwa machache au ikiwa kwa mengi, si wewe tu ila na hao wote wanaonisikia leo wawe kama mimi, isipokuwa kuwa katika minyororo hii.


Upendo huvumilia, hufadhili; upendo hauhusudu; upendo hautakabari; haujivuni;


Nami nataka ninyi nyote mnene kwa lugha, lakini zaidi sana mpate kutoa unabii, maana yeye atoaye unabii ni mkuu kuliko yeye anenaye kwa lugha, isipokuwa afasiri, ili kusudi kanisa lipate kujengwa.


Basi, mtu yeyote na asijisifie wanadamu. Kwa maana vyote ni vyenu;


kwa maana hata sasa ninyi ni watu wa tabia ya mwilini. Maana, ikiwa kwenu kuna husuda na fitina, je! Si watu wa tabia ya mwilini ninyi; tena mnaenenda kwa jinsi ya kibinadamu?


Msitende neno lolote kwa kushindana wala kwa majivuno; bali kwa unyenyekevu, kila mtu na amhesabu mwenziwe kuwa bora kuliko nafsi yake.


Au mwadhani ya kwamba Maandiko yasema bure? Huyo Roho akaaye ndani yetu hututamani kiasi cha kuona wivu?


Ndugu, msinung'unikiane, msije mkahukumiwa. Angalieni, mwamuzi amesimama mbele ya milango.


Basi, wekeni mbali uovu wote na hila yote, na unafiki na husuda na masingizio yote.


na Roho ya BWANA itakujia kwa nguvu, nawe utatabiri pamoja nao, nawe utageuzwa kuwa mtu mwingine.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo