Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Hesabu 1:51 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC

51 Tena hapo maskani itakapokwenda mbele, Walawi wataishusha; tena hapo maskani itakaposimamishwa, Walawi wataisimamisha; na mgeni atakayekaribia atauawa.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

51 Tena wakati wa hema kungolewa Walawi ndio watakaolingoa na wakati wa hema kusimikwa Walawi ndio watakaolisimamisha.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

51 Tena wakati wa hema kungolewa Walawi ndio watakaolingoa na wakati wa hema kusimikwa Walawi ndio watakaolisimamisha.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

51 Tena wakati wa hema kung'olewa Walawi ndio watakaoling'oa na wakati wa hema kusimikwa Walawi ndio watakaolisimamisha.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

51 Wakati wowote Maskani inapohamishwa, Walawi wataifungua, na wakati wowote Maskani inapotakiwa kusimamishwa, Walawi watafanya kazi hiyo. Mtu yeyote mwingine ambaye atasogea karibu nayo atauawa.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

51 Wakati wowote Maskani inapohamishwa, Walawi wataifungua, na wakati wowote maskani inapotakiwa kusimamishwa, Walawi watafanya kazi hiyo. Mtu yeyote mwingine ambaye atasogea karibu nayo atauawa.

Tazama sura Nakili




Hesabu 1:51
15 Marejeleo ya Msalaba  

Ndipo hasira ya BWANA ikawaka juu ya Uza; naye Mungu akampiga huko kwa kosa lake; hata akafa pale pale penye sanduku la Mungu.


Ikawa mwaka wa pili, mwezi wa pili, siku ya ishirini ya mwezi, hilo wingu liliinuka kutoka pale juu ya maskani ya ushahidi.


viwe ukumbusho kwa wana wa Israeli, ili mgeni yeyote asiye wa kizazi cha Haruni, asikaribie kufukiza uvumba mbele za BWANA; asiwe mfano wa Kora, na mkutano wake; kama BWANA alivyonena naye, kwa kupitia kwa Musa.


Kila mtu akaribiaye, aikaribiaye maskani ya BWANA, hufa; je! Tutakufa sote pia?


Kisha itakuwa, mtu huyo nitakayemchagua, fimbo yake itachipuka nami nitayakomesha manung'uniko ya wana wa Israeli, wanung'unikiayo kwangu juu yenu.


Mwanzo wa sasa wana wa Israeli wasikaribie hema ya kukutania, wasije wakachukua dhambi, nao wakafa.


Nao watahudumu kwa kufuata amri yako, na kuhudumu hemani pote; lakini wasikaribie vyombo vya patakatifu, wala madhabahu, wasife, wao pamoja na ninyi.


Nao watataambatana nawe, na kuhudumu katika hema ya kukutania, kwa ajili ya huduma yote ya hema; na mgeni asiwakaribie ninyi.


Nawe na wanao pamoja nawe mtautunza ukuhani wenu, kwa ajili ya kila kitu cha madhabahu, na kwa ajili ya vile vilivyomo ndani ya pazia, nanyi mtatumika. Nawapeni ukuhani kuwa utumishi wa kipawa; na mgeni akaribiaye atauawa.


Nawe utawaweka Haruni na wanawe, nao wataushika ukuhani wao, na mgeni atakayekaribia atauawa.


Na hao watakaopanga mbele ya maskani upande wa mashariki, mbele ya hema ya kukutania upande wa kuelekea maawio ya jua, watakuwa hawa, Musa na Haruni na wanawe, wenye kulinda ulinzi wa mahali patakatifu, yaani, huo ulinzi wa wana wa Israeli; na mgeni atakayekaribia atauawa.


Basi BWANA aliwapiga baadhi ya watu wa Beth-shemeshi, kwa sababu wamechungulia ndani ya hilo sanduku la BWANA, wapata watu sabini, na watu elfu hamsini; nao watu wakalalamika, kwa kuwa BWANA amewapiga watu kwa uuaji mkuu.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo