Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -




Habakuki 2:6 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC

6 Je! Hawa wote hawatapiga mfano juu yake, na mithali ya kusimanga juu yake, wakisema, Ole wake yeye aongezaye kisicho mali yake! Hata lini? Na ole wake yeye ajitwikaye mzigo wa rehani!

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

6 Kila mtu atamdhihaki mtu wa namna hiyo na kumtungia misemo ya dhihaka: “Ole wako unayejirundikia visivyo vyako, na kuchukua rehani mali za watu lakini hulipi! Utaendelea kufanya hivyo hadi lini?

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

6 Kila mtu atamdhihaki mtu wa namna hiyo na kumtungia misemo ya dhihaka: “Ole wako unayejirundikia visivyo vyako, na kuchukua rehani mali za watu lakini hulipi! Utaendelea kufanya hivyo hadi lini?

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

6 Kila mtu atamdhihaki mtu wa namna hiyo na kumtungia misemo ya dhihaka: “Ole wako unayejirundikia visivyo vyako, na kuchukua rehani mali za watu lakini hulipi! Utaendelea kufanya hivyo hadi lini?

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

6 “Je, watu wote hawatamsuta kwa dhihaka na kumbeza, wakisema, “ ‘Ole wake yeye akusanyaye bidhaa zilizoibwa na kujifanyia utajiri kwa kutoza kwa nguvu! Ataendelea hivi kwa muda gani?’

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

6 “Je, watu wote hawatamsuta kwa dhihaka na kumbeza, wakisema, “ ‘Ole wake yeye akusanyaye bidhaa zilizoibwa na kujifanyia utajiri kwa kutoza kwa nguvu! Ataendelea hivi kwa muda gani?’

Tazama sura Nakili




Habakuki 2:6
25 Marejeleo ya Msalaba  

BWANA, hadi lini wasio haki, Hadi lini wasio haki watashangilia?


Yeye awaoneaye maskini ili kuongeza mapato, Naye ampaye tajiri, hupata hasara.


Kwa maana amesema, Kwa nguvu za mkono wangu nimetenda jambo hili, na kwa hekima yangu; maana mimi nina busara; nami nimeiondoa mipaka ya watu, nikaziteka akiba zao, nikawaangusha waketio juu ya viti vya enzi kama afanyavyo shujaa.


Hula majivu; moyo uliodanganyika umempotosha, asiweze kuiokoa nafsi yake, wala kusema, Je! Sio uongo mkononi mwangu?


Ole wao waongezao nyumba baada ya nyumba, na kuweka shamba karibu na shamba, hadi ikawa hapana nafasi tena, nanyi ikawa hamna budi kukaa peke yenu katikati ya nchi!


Kwa nini mtoe fedha kwa ajili ya kitu ambacho si chakula? Na mapato yenu kwa kitu kisichoshibisha? Nisikilizeni kwa bidii, mle kilicho chema, Na kujifurahisha nafsi zenu kwa unono.


Kama kware akusanyaye makinda asiyoyaangua, ndivyo alivyo mtu ajipatiaye mali, wala si kwa haki, katikati ya maisha yake itamtoka, na mwisho wake atakuwa mpumbavu.


Tena kwa ajili yao laana itatumiwa na wafungwa wote wa Yuda, walioko Babeli, kusema, BWANA akufanye uwe kama Sedekia, na kama Ahabu, ambao mfalme wa Babeli aliwaoka motoni;


Kwa sababu ya ghadhabu ya BWANA haitakaliwa na mtu, bali itakuwa ukiwa mtupu; kila mtu apitaye karibu na Babeli atashangaa, atazomea kwa sababu ya mapigo yake yote.


Walio hodari watasema naye, toka kati ya kuzimu pamoja nao wamsaidiao; wameshuka wamelala kimya, hata wasiotahiriwa, wakiwa wameuawa kwa upanga.


Siku hiyo watatunga mithali juu yenu, na kuomboleza kwa maombolezo ya huzuni nyingi, na kusema, Sisi tumeangamizwa kabisa; Yeye analibadili fungu la watu wangu; Jinsi anavyoniondolea hilo! Awagawia waasi mashamba yetu.


Yeye huwatoa wote kwa ndoana yake, huwakamata katika wavu wake, na kuwakusanya katika juya lake; ndiyo sababu afurahi na kupendezwa.


Ole wake yeye ajengaye mji kwa damu, awekaye imara mji mkubwa kwa uovu!


Angalieni; je! Jambo hili halikutoka kwa BWANA wa majeshi, kwamba watu wajishughulikie moto, na mataifa wajisumbue kwa ajili ya ubatili?


Naye akatunga mithali yake, akasema, Ondoka Balaki, ukasikilize; Nisikilize, Ee mwana wa Sipori;


Akatunga mithali yake, akasema, Balaki amenileta kutoka Aramu, Mfalme wa Moabu kutoka milima ya mashariki, Njoo! Unilaanie Yakobo, Njoo! Unishutumie Israeli.


Lakini Mungu akamwambia, Mpumbavu wewe, usiku huu wa leo wanataka roho yako! Na vitu ulivyojiwekea tayari vitakuwa vya nani?


Lakini mwisho wa mambo yote umekaribia; basi, iweni na akili, mkeshe katika sala.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo