Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -




Habakuki 2:13 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC

13 Angalieni; je! Jambo hili halikutoka kwa BWANA wa majeshi, kwamba watu wajishughulikie moto, na mataifa wajisumbue kwa ajili ya ubatili?

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

13 Mwenyezi-Mungu wa majeshi husababisha juhudi za watu zipotelee motoni, na mataifa yajishughulishe bure.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

13 Mwenyezi-Mungu wa majeshi husababisha juhudi za watu zipotelee motoni, na mataifa yajishughulishe bure.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

13 Mwenyezi-Mungu wa majeshi husababisha juhudi za watu zipotelee motoni, na mataifa yajishughulishe bure.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

13 Je, Mwenyezi Mungu, Mungu wa majeshi ya mbinguni hakuonesha kwamba kazi ya wanadamu ni mafuta tu kwa ajili ya moto, na kwamba mataifa yanajichosha bure?

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

13 Je, bwana Mwenye Nguvu Zote hakuonyesha kwamba kazi ya wanadamu ni mafuta tu kwa ajili ya moto, na kwamba mataifa yanajichosha bure?

Tazama sura Nakili




Habakuki 2:13
12 Marejeleo ya Msalaba  

Mtu mmoja akamwambia Daudi ya kwamba, Ahithofeli yu katika hao waliopatana na Absalomu; Daudi akasema, Ee BWANA, nakusihi, uugeuze ushauri wa Ahithofeli uwe ubatili.


Kweli, watu wote hupita kama kivuli; Wao hujisumbua bure tu; Wanajirundikia mali wala hawajui ni nani atakayeirithi.


Hapana hekima, wala ufahamu, Wala shauri, juu ya BWANA.


Tazama, ninyi nyote mwashao moto, mjifungiao hiyo mienge; endeni ninyi katika muali wa moto wenu, na katikati ya mienge mliyoiwasha. Mtayapata haya kwa mkono wangu; mtalala kwa huzuni.


Kwa nini mtoe fedha kwa ajili ya kitu ambacho si chakula? Na mapato yenu kwa kitu kisichoshibisha? Nisikilizeni kwa bidii, mle kilicho chema, Na kujifurahisha nafsi zenu kwa unono.


BWANA wa majeshi asema hivi, Kuta pana za Babeli zitabomolewa kabisa, na malango yake marefu yatateketezwa; nao watu watajitaabisha kwa ubatili, na mataifa kwa moto; nao watachoka.


nawe utasema, Hivyo ndivyo utakavyozama Babeli, wala hautazuka tena, kwa sababu ya mabaya yote nitakayoleta juu yake; nao watachoka. Maneno ya Yeremia yamefika hata hapa.


Ijapokuwa Edomu asema, Tumepondwapondwa, lakini tutarudi na kupajenga mahali palipoachwa hali ya ukiwa; BWANA wa majeshi asema hivi, Wao watajenga, bali mimi nitaangusha; na watu watawaita, Mpaka wa uovu, na, Watu ambao BWANA anawaghadhabikia milele.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo