Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -




Habakuki 2:12 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC

12 Ole wake yeye ajengaye mji kwa damu, awekaye imara mji mkubwa kwa uovu!

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

12 “Ole wako unayejenga mji kwa mauaji unayesimika jiji kwa maovu!

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

12 “Ole wako unayejenga mji kwa mauaji unayesimika jiji kwa maovu!

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

12 “Ole wako unayejenga mji kwa mauaji unayesimika jiji kwa maovu!

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

12 “Ole wake yeye ajengaye mji kwa kumwaga damu na kuusimamisha mji kwa uhalifu!

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

12 “Ole wake yeye ajengaye mji kwa kumwaga damu na kuusimamisha mji kwa uhalifu!

Tazama sura Nakili




Habakuki 2:12
12 Marejeleo ya Msalaba  

Katika siku zake, Hieli Mbetheli akajenga Yeriko; akatia misingi yake kwa kufiwa na Abiramu mzaliwa wake wa kwanza, na kuyaweka malango yake kwa kufiwa na mwana wake mdogo Segubu; sawasawa na neno la BWANA alilolinena kwa Yoshua mwana wa Nuni.


Basi Bwana MUNGU asema hivi; Ole wake mji wa damu! Mimi nami nitaiongeza chungu.


Wanaoijenga Sayuni kwa damu, na Yerusalemu kwa uovu.


Ole wake mji wa damu! Umejaa mambo ya uongo na unyang'anyi; mateka hayaondoki.


Je! Hawa wote hawatapiga mfano juu yake, na mithali ya kusimanga juu yake, wakisema, Ole wake yeye aongezaye kisicho mali yake! Hata lini? Na ole wake yeye ajitwikaye mzigo wa rehani!


Basi Yeye atufanyaye imara pamoja nanyi katika Kristo, na kututia mafuta, ni Mungu,


Naye Yoshua akawaapisha kiapo wakati ule, akasema, Na alaaniwe na BWANA mtu yule atakayeinuka na kutaka kuujenga tena mji huu wa Yeriko; atakayeweka msingi wake mzaliwa wake wa kwanza na afe. Tena atakayesimamisha malango yake mtoto wake wa kiume aliye mdogo na afe.


Nikamwona yule mwanamke amelewa kwa damu ya watakatifu, na kwa damu ya mashahidi wa Yesu. Nami nilipomwona nikastaajabu sana.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo