Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -




Habakuki 1:10 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC

10 Naam, huwadhihaki wafalme, na wakuu ni kitu cha kudharauliwa kwake; huidharau kila ngome; kwa maana huirundikia udongo, na kuitwaa.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

10 Wanawadhihaki wafalme, na kuwadharau watawala. Kila ngome kwao ni mzaha, wanairundikia udongo na kuiteka.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

10 Wanawadhihaki wafalme, na kuwadharau watawala. Kila ngome kwao ni mzaha, wanairundikia udongo na kuiteka.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

10 Wanawadhihaki wafalme, na kuwadharau watawala. Kila ngome kwao ni mzaha, wanairundikia udongo na kuiteka.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

10 Wanawabeza wafalme, na kuwadhihaki watawala. Wanaicheka miji yote yenye ngome; wanalundika udongo na kuiteka hiyo miji.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

10 Wanawabeza wafalme, na kuwadhihaki watawala. Wanaicheka miji yote iliyozungushiwa maboma; wanafanya malundo ya udongo na kuiteka hiyo miji.

Tazama sura Nakili




Habakuki 1:10
14 Marejeleo ya Msalaba  

Na Yekonia, mfalme wa Yuda, akatoka akamwendea mfalme wa Babeli, yeye na mama yake, na watumishi wake, na wakuu wa watu wake, na maofisa wake; mfalme wa Babeli akamchukua mateka katika mwaka wa nane wa kutawala kwake.


Mwaka ulipokwisha, Nebukadneza akatuma wajumbe, akamchukua mpaka Babeli; pamoja na vyombo vya thamani vya nyumba ya BWANA; akamtawaza Sedekia nduguye awe mfalme juu ya Yuda na Yerusalemu.


Juu yake akakwea Nebukadneza, mfalme wa Babeli, akamfunga kwa pingu, amchukue mpaka Babeli.


Je! Kalno si kama Karkemishi? Hamathi si kama Arpadi? Samaria si kama Dameski?


Wao wakuonao watakukazia macho, Watakuangalia sana, wakisema, Je! Huyu ndiye aliyeitetemesha dunia, Huyu ndiye aliyetikisa falme;


Yuko wapi mfalme wa Hamathi, na mfalme wa Arpadi, na mfalme wa mji wa Sefarvaimu, wa Hena, na wa Iva?


Maana BWANA asema hivi, Tumesikia sauti ya tetemeko, na ya hofu, wala si ya amani.


angalia maboma haya; wameujia mji huu ili kuutwaa; na mji huu umetiwa katika mikono ya Wakaldayo wanaopigana nao, kwa sababu ya upanga, na njaa, na tauni; na hayo uliyosema yamekuwa; na, tazama, wewe unayaona.


Maana BWANA, Mungu wa Israeli asema hivi, kuhusu nyumba za mji huu, na kuhusu nyumba za wafalme wa Yuda, zilizobomolewa ili kuyapinga maboma na upanga;


Nami nitamwaga ghadhabu yangu juu yako; nitakupulizia moto wa hasira yangu; nami nitakutia katika mikono ya watu walio kama hayawani, wajuao sana kuangamiza.


Atawaua binti zako kwa upanga katika mashamba; naye atafanya ngome juu yako, na kufanya maboma juu yako, na kuiinua ngao juu yako.


Na itakuwa, katika siku ile ya dhabihu ya BWANA, nitawaadhibu wakuu, na wana wa mfalme, na watu wote waliovaa mavazi ya kigeni.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo