Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -

Ezra 8:35 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC

35 Na wana wa uhamisho, waliokuwa wametoka katika uhamisho wakamtolea Mungu wa Israeli sadaka za kuteketezwa, ng'ombe kumi na wawili kwa ajili ya Israeli wote, na kondoo dume tisini na sita, na wana-kondoo sabini na saba, na mabeberu kumi na wawili, kuwa sadaka ya dhambi, hao wote pia walikuwa sadaka ya kuteketezwa kwa BWANA.

Tazama sura Nakili

Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

35 Kisha, watu wote waliorudi kutoka uhamishoni walimtolea Mungu wa Israeli sadaka zao za kuteketezwa. Walitoa mafahali 12 kwa ajili ya Israeli yote, kondoo madume 96 na wanakondoo 77; pia walitoa mbuzi 12 kama sadaka ya kuondoa dhambi. Wanyama wote hawa walitolewa kuwa sadaka ya kuteketezwa kwa Mwenyezi-Mungu.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

35 Kisha, watu wote waliorudi kutoka uhamishoni walimtolea Mungu wa Israeli sadaka zao za kuteketezwa. Walitoa mafahali 12 kwa ajili ya Israeli yote, kondoo madume 96 na wanakondoo 77; pia walitoa mbuzi 12 kama sadaka ya kuondoa dhambi. Wanyama wote hawa walitolewa kuwa sadaka ya kuteketezwa kwa Mwenyezi-Mungu.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

35 Kisha mateka waliokuwa wamerudi kutoka utumwani wakatoa sadaka za kuteketezwa kwa moto kwa Mungu wa Israeli: mafahali kumi na wawili kwa ajili ya Israeli wote, kondoo dume tisini na sita, wana-kondoo sabini na saba, na beberu kumi na wawili kuwa sadaka ya dhambi. Hii yote ilikuwa sadaka ya kuteketezwa kwa moto kwa Mwenyezi Mungu.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

35 Kisha mateka waliokuwa wamerudi kutoka utumwani wakatoa sadaka za kuteketezwa kwa moto kwa Mungu wa Israeli: mafahali kumi na wawili kwa ajili ya Israeli wote, kondoo dume tisini na sita, wana-kondoo sabini na saba na mbuzi dume kumi na wawili kuwa sadaka ya dhambi. Hii yote ilikuwa sadaka ya kuteketezwa kwa moto kwa bwana.

Tazama sura Nakili

Ezra 8:35
9 Marejeleo ya Msalaba  

Basi hawa ndio watu wa mkoa, waliokwea kutoka katika ule uhamisho wa hao waliokuwa wamechukuliwa, ambao Nebukadneza, mfalme wa Babeli, aliwachukua mateka mpaka Babeli, nao wakarudi Yerusalemu na Yuda, kila mtu mjini kwake;

Na katika kuiweka wakfu nyumba ya Mungu, wakatoa sadaka, ng'ombe mia moja, na kondoo dume mia mbili, na wana-kondoo mia nne; tena wakatoa mbuzi dume kumi na wawili, kuwa sadaka ya dhambi kwa ajili ya Waisraeli wote, kwa hesabu ya makabila ya Israeli.

vile vyombo vyote kwa hesabu na kwa uzani; tena uzani wake wote uliandikwa wakati ule.

na ng'ombe dume mchanga mmoja, na kondoo dume mmoja, na mwana-kondoo dume mmoja wa mwaka mmoja, kuwa sadaka ya kuteketezwa;

Tufuate:

Matangazo

Matangazo