Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Ezra 8:28 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC

28 Kisha nikawaambia, Ninyi mmekuwa watakatifu kwa BWANA, na hivyo vyombo ni vitakatifu; na fedha na dhahabu ni matoleo ya hiari kwa BWANA, Mungu wa baba zenu.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

28 Kisha nikawaambia, “Nyinyi ni wakfu kwa Mwenyezi-Mungu. Kadhalika vyombo ni wakfu na fedha na dhahabu ni matoleo ya hiari kwa Mwenyezi-Mungu, Mungu wa babu zenu.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

28 Kisha nikawaambia, “Nyinyi ni wakfu kwa Mwenyezi-Mungu. Kadhalika vyombo ni wakfu na fedha na dhahabu ni matoleo ya hiari kwa Mwenyezi-Mungu, Mungu wa babu zenu.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

28 Kisha nikawaambia, “Nyinyi ni wakfu kwa Mwenyezi-Mungu. Kadhalika vyombo ni wakfu na fedha na dhahabu ni matoleo ya hiari kwa Mwenyezi-Mungu, Mungu wa babu zenu.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

28 Niliwaambia, “Ninyi pamoja na vyombo hivi ni wakfu kwa Mwenyezi Mungu. Fedha na dhahabu ni sadaka ya hiari kwa Mwenyezi Mungu, Mungu wa baba zenu.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

28 Niliwaambia, “Ninyi pamoja na vyombo hivi ni wakfu kwa bwana. Fedha na dhahabu ni sadaka ya hiari kwa bwana, Mungu wa baba zenu.

Tazama sura Nakili




Ezra 8:28
15 Marejeleo ya Msalaba  

Kwani kazi yao ilikuwa kuwangojea wana wa Haruni katika utumishi wa nyumba ya BWANA, nyuani, na vyumbani, na kwa kuvisafisha vitakatifu vyote, ndiyo kazi ya utumishi wa nyumba ya Mungu;


Na katika Walawi; Ahia mtunzaji wa hazina ya nyumba ya Mungu, pamoja na hazina ya vitu vilivyowekwa wakfu.


Nao walipomaliza, wakaleta mbele ya mfalme na Yehoyada fedha iliyobaki, na kwavyo vikafanywa vyombo vya nyumba ya BWANA, vyombo vya utumishi, navyo vya kutolea, na miiko, na vyombo vya dhahabu na fedha. Wakatoa sadaka za kuteketezwa katika nyumba ya BWANA, mara kwa mara, siku zote za Yehoyada.


na mabakuli ishirini ya dhahabu, thamani yake darkoni elfu moja; na vyombo viwili vya shaba nzuri iliyong'aa, thamani yake sawa na dhahabu.


Wana wa Israeli wakaleta sadaka za kumpa BWANA kwa moyo wa kupenda; wote, wanaume kwa wanawake, ambao mioyo yao iliwafanya kuwa wapenda kuleta kwa hiyo kazi, ambayo BWANA aliamuru ifanywe kwa mkono wa Musa.


Nendeni zenu, nendeni zenu, tokeni huko, msiguse kitu kichafu; tokeni kati yake; iweni safi ninyi mnaochukua vyombo vya BWANA.


na matoleo yake yalikuwa sahani moja ya fedha, uzani wake ni shekeli mia moja na thelathini, na bakuli moja ya fedha uzani wake ni shekeli sabini, kwa shekeli ya mahali patakatifu; vyombo hivyo vyote viwili vilikuwa vimejaa unga mwembamba uliochanganywa na mafuta kuwa sadaka ya unga;


Akamnena Lawi, Thumimu yako na Urimu yako vina mtakatifu wako, Uliyemjaribu huko Masa; Ukateta naye kwenye maji ya Meriba.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo