Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -




Ezra 10:19 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC

19 Nao wakatoa ahadi ya kwamba wataachana na wake zao; na kwa kuwa walikuwa na hatia, wakatoa kondoo dume kwa hatia yao.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

19 Hao waliahidi kuwaacha wake zao, na wakatoa kondoo dume kuwa sadaka kwa ajili ya hatia yao.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

19 Hao waliahidi kuwaacha wake zao, na wakatoa kondoo dume kuwa sadaka kwa ajili ya hatia yao.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

19 Hao waliahidi kuwaacha wake zao, na wakatoa kondoo dume kuwa sadaka kwa ajili ya hatia yao.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

19 (Wote walitoa nadhiri kwa kuandika kwa mikono yao kuwafukuza wake zao, kwa hatia yao, kila mmoja akatoa kondoo dume kutoka kundini mwake kuwa sadaka ya hatia.)

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

19 (Wote walitoa nadhiri kwa kuandika kwa mikono yao kuwafukuza wake zao, kwa hatia yao, kila mmoja akatoa kondoo dume kutoka kundini mwake kama sadaka ya hatia.)

Tazama sura Nakili




Ezra 10:19
9 Marejeleo ya Msalaba  

Alipotoka huko akamkuta Yehonadabu mwana wa Rekabu akija kumlaki; akamsalimu akamwambia, Je! Moyo wako umenyoka, kama moyo wangu ulivyo pamoja na moyo wako? Akajibu Yehonadabu, Ndio. Yehu akamwambia, Kama ndio, nipe mkono wako. Akampa mkono, akamkalisha pamoja naye garini.


Nao wakuu wote, na mashujaa, na wana wote wa mfalme Daudi nao, wakaahidi kuwa watiifu kwa mfalme Sulemani.


Msiwe sasa wenye shingo ngumu kama baba zenu; lakini mjitoe kwa BWANA, mkaingie katika patakatifu pake, alipopatakasa milele, mkamtumikie BWANA, Mungu wenu, hasira yake kali iwageukie mbali.


Na wa wazawa wa Imeri; Hanani, na Zebadia.


Tumewapa hao Wamisri mkono; Na Waashuri nao, ili tushibe chakula.


ndipo itakapokuwa, akiwa amefanya dhambi, na kupata hatia, atarudisha hicho alichokipata kwa kunyang'anya, au kitu kile alichokipata kwa kuonea, au ile amana aliyowekewa, au kitu kile kilichopotea alichokipata yeye,


Kisha ataleta sadaka yake ya hatia kwa BWANA, ni kondoo dume wa katika kundi lake, mkamilifu, sawasawa na hesabu utakayomwandikia, kuwa sadaka ya hatia, na kumpa kuhani;


tena Yakobo, Kefa, na Yohana, waliosifika kuwa ni nguzo, walipoitambua ile neema niliyopewa, walinipa mimi na Barnaba mkono wa kulia wa kuonesha ushirikiano; ili sisi tuende kwa Mataifa, na wao waende kwa watu wa tohara;


Tufuate:

Matangazo


Matangazo