Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -




Ezra 10:14 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC

14 Basi wakuu wetu na wawekwe kwa ajili ya mkutano wote, na watu wote walio katika miji yetu, waliooa wanawake wageni, na waje nyakati zilizoamriwa, tena pamoja nao na waje wazee wa kila mji, na waamuzi wa miji hiyo, hata ghadhabu kali ya Mungu wetu itakapoondolewa mbali, jambo hili likamalizike.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

14 Afadhali maofisa wetu wabaki Yerusalemu kushughulikia jambo hili kwa niaba ya watu wote. Kisha, kila mmoja ambaye ameoa mwanamke wa kigeni na aje kwa zamu pamoja na viongozi na mahakimu wa mji wake, mpaka hapo ghadhabu kali ya Mungu wetu itakapoondolewa kwetu.”

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

14 Afadhali maofisa wetu wabaki Yerusalemu kushughulikia jambo hili kwa niaba ya watu wote. Kisha, kila mmoja ambaye ameoa mwanamke wa kigeni na aje kwa zamu pamoja na viongozi na mahakimu wa mji wake, mpaka hapo ghadhabu kali ya Mungu wetu itakapoondolewa kwetu.”

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

14 Afadhali maofisa wetu wabaki Yerusalemu kushughulikia jambo hili kwa niaba ya watu wote. Kisha, kila mmoja ambaye ameoa mwanamke wa kigeni na aje kwa zamu pamoja na viongozi na mahakimu wa mji wake, mpaka hapo ghadhabu kali ya Mungu wetu itakapoondolewa kwetu.”

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

14 Maafisa wetu na watende kwa niaba ya kusanyiko lote. Kisha kila mmoja katika miji yetu ambaye ameoa mwanamke wa kigeni aje kwa wakati uliopangwa, akiwa pamoja na wazee na waamuzi wa kila mji, hadi hasira kali ya Mungu wetu katika shauri hili itakapoondolewa kwetu.”

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

14 Maafisa wetu na wafanye kwa niaba ya kusanyiko lote. Kisha kila mmoja katika miji yetu ambaye ameoa mwanamke wa kigeni aje kwa wakati uliopangwa, akiwa pamoja na wazee na waamuzi wa kila mji, hadi hasira kali ya Mungu wetu katika shauri hili itakapoondolewa kwetu.”

Tazama sura Nakili




Ezra 10:14
14 Marejeleo ya Msalaba  

Lakini BWANA hakuuacha ukali wa ghadhabu yake nyingi, ambayo kwayo hasira yake iliwaka juu ya Yuda, kwa sababu ya machukizo yote ambayo Manase amemchukiza.


Haya, nisikieni mimi basi, mwarudishe wafungwa, mliowachukua mateka wa ndugu zenu; kwa maana ghadhabu ya BWANA iliyo kali iko juu yenu.


Basi nia yangu ni kufanya agano na BWANA, Mungu wa Israeli, ili kwamba hasira yake kali itugeukie mbali.


Msiwe sasa wenye shingo ngumu kama baba zenu; lakini mjitoe kwa BWANA, mkaingie katika patakatifu pake, alipopatakasa milele, mkamtumikie BWANA, Mungu wenu, hasira yake kali iwageukie mbali.


Lakini watu hawa ni wengi, tena ni wakati wa mvua nyingi, nasi hatuwezi kusimama nje, tena kazi hii si kazi ya siku moja, wala ya siku mbili; maana tumekosa sana katika jambo hili.


Yonathani, mwana wa Asaheli, na Yazeya, mwana wa Tikwa, hawa peke yao ndio waliosimama kulipinga neno hilo; na Meshulamu, na Shabethai Mlawi, wakawasaidia.


Lakini Yeye, kwa kuwa anayo rehema, Husamehe uovu wala haangamizi. Mara nyingi huipishia mbali ghadhabu yake, Wala haiwashi hasira yake yote.


Na katika siku hiyo utasema, Ee BWANA, nitakushukuru wewe; Kwa kuwa ijapokuwa ulinikasirikia, Hasira yako imegeukia mbali, Nawe unanifariji moyo.


Kisha BWANA akamwambia Musa, Watwae wakuu wote wa watu hao, uwanyongee juani mbele ya BWANA ili kwamba hizo hasira kali za BWANA ziwaondokee Israeli.


Kisishikamane na mkono wako kitu chochote katika kitu kilichoharimishwa; ili ageuke BWANA na ukali wa hasira zake akurehemu, akuonee huruma, na kukufanya kuwa wengi, kama alivyowaapia baba zako;


uwaendee makuhani Walawi, na mwamuzi atakayekuwako siku hizo; uwaulize; nao watakuonesha hukumu ya maamuzi;


Kisha wakakusanya juu yake rundo kubwa la mawe hata leo; naye BWANA akauacha ukali wa hasira yake. Kwa sababu hiyo jina la mahali pale likaitwa, Bonde la Akori, hata leo.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo