Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Ezekieli 8:15 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC

15 Akaniambia, Mwanadamu umeyaona haya? Utaona tena machukizo makubwa kuliko hayo.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

15 Mungu akaniambia: “Wewe mtu, umeyaona hayo? Bado utaona machukizo mengine makubwa kuliko hayo.”

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

15 Mungu akaniambia: “Wewe mtu, umeyaona hayo? Bado utaona machukizo mengine makubwa kuliko hayo.”

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

15 Mungu akaniambia: “Wewe mtu, umeyaona hayo? Bado utaona machukizo mengine makubwa kuliko hayo.”

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

15 Akaniambia, “Je, mwanadamu, unaliona hili? Utayaona mambo yanayochukiza hata zaidi.”

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

15 Akaniambia, “Unaliona hili, mwanadamu? Utaona vitu ambavyo ni machukizo kuliko hili.”

Tazama sura Nakili




Ezekieli 8:15
7 Marejeleo ya Msalaba  

Kwa sababu hiyo, kama mimi niishivyo, asema Bwana MUNGU, hakika kwa kuwa umepatia unajisi patakatifu pangu, kwa matendo yako yote niyachukiayo, na kwa machukizo yako yote, kwa sababu hiyo mimi nami nitakupunguza; wala jicho langu halitaachilia, wala sitaona huruma.


Ndipo akanileta mpaka maingilio ya lango la kaskazini mwa nyumba ya BWANA, ulioelekea upande wa kaskazini, na tazama, wanawake wameketi wakimlilia Tamuzi.


Akanileta mpaka ua wa ndani wa nyumba ya BWANA, na tazama, mlangoni pa hekalu la BWANA, kati ya ukumbi na madhabahu, walikuwako watu kama ishirini na watano, wamelipa kisogo hekalu la BWANA, na nyuso zao zimeelekea upande wa mashariki, nao wanaliabudu jua, kwa kuuelekea upande wa mashariki.


Akaniambia, Mwanadamu, je! Unayaona wanayoyafanya, yaani, haya machukizo makubwa wanayoyafanya nyumba ya Israeli hapa, ili niende zangu mbali na patakatifu pangu? Lakini utaona tena machukizo makubwa mengine.


Akaniambia, Ingia uyaone machukizo mabaya wanayoyafanya hapa.


Lakini watu waovu na wadanganyaji wataendelea, na kuzidi kuwa waovu, wakidanganya na kudanganyika.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo