Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Ezekieli 8:12 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC

12 Kisha akaniambia, Mwanadamu, umeyaona wanayotenda wazee wa nyumba ya Israeli gizani, kila mtu ndani ya vyumba vyake vya sanamu? Maana husema, BWANA hatuoni; BWANA ameiacha nchi hii.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

12 Kisha Mungu akaniambia, “Wewe mtu, umeona wanayotenda wazee wa Waisraeli gizani, kila mtu katika chumba chake cha sanamu. Wanadai ati Mwenyezi-Mungu hatuoni. Mwenyezi-Mungu ameiacha nchi.”

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

12 Kisha Mungu akaniambia, “Wewe mtu, umeona wanayotenda wazee wa Waisraeli gizani, kila mtu katika chumba chake cha sanamu. Wanadai ati Mwenyezi-Mungu hatuoni. Mwenyezi-Mungu ameiacha nchi.”

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

12 Kisha Mungu akaniambia, “Wewe mtu, umeona wanayotenda wazee wa Waisraeli gizani, kila mtu katika chumba chake cha sanamu. Wanadai ati Mwenyezi-Mungu hatuoni. Mwenyezi-Mungu ameiacha nchi.”

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

12 Akaniambia, “Mwanadamu, umeona wanayoyafanya wazee wa Israeli wakiwa gizani, kila mmoja kwenye mahali pa ibada pa sanamu yake? Wao husema, ‘Mwenyezi Mungu hatuoni, Mwenyezi Mungu ameiacha nchi.’ ”

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

12 Akaniambia, “Mwanadamu, umeona wanayoyafanya wazee wa nyumba ya Israeli gizani, kila mmoja kwenye sehemu yake mwenyewe ya kufanyia ibada za sanamu yake? Wao husema, ‘bwana hatuoni, bwana ameiacha nchi.’ ”

Tazama sura Nakili




Ezekieli 8:12
21 Marejeleo ya Msalaba  

Tena, wana wa Israeli wakafanya kwa siri mambo yasiyokuwa mema juu ya BWANA, Mungu wao, wakajijengea mahali pa juu katika miji yao yote, kutoka mnara wa walinzi hata katika miji yenye boma.


Asema moyoni mwake, Mungu amesahau, Auficha uso wake, haoni kamwe.


Mpumbavu husema moyoni, Hakuna Mungu; Wameharibu matendo yao na kuyafanya chukizo, Hakuna atendaye mema.


Nao husema, Mungu ajuaje? Yako maarifa kwake aliye juu?


Ole wao wanaojitahidi kumficha BWANA mashauri yao, na matendo yao yamo gizani, nao husema, Ni nani atuonaye? Nani atujuaye?


Maana umeutumainia ubaya wako; umesema, Hapana anionaye; hekima yako, na maarifa yako yamekupotosha, nawe umesema moyoni mwako, Mimi ndiye, wala hapana mwingine zaidi yangu mimi.


Ndipo baadhi ya wazee wa Israeli wakanijia, wakaketi mbele yangu.


Ikawa katika mwaka wa saba, mwezi wa tano, siku ya kumi ya mwezi, baadhi ya wazee wa Israeli walikuja ili kuuliza kwa BWANA, wakaketi mbele yangu.


Na watu sabini wa wazee wa Israeli walikuwa wamesimama na kuzielekea, na katikati yao alisimama Yaazania, mwana wa Shafani; kila mmoja ana chetezo mkononi mwake, na harufu ya moshi wa uvumba ilipaa juu.


Akaniambia tena, Utaona tena machukizo makubwa mengine wanayoyatenda.


Akaniambia, Mwanadamu umeyaona haya? Utaona tena machukizo makubwa kuliko hayo.


Basi, akaniambia, Umeyaona haya, Ee mwanadamu? Je! Ni jambo dogo sana kwa nyumba ya Yuda, wayafanye machukizo wanayoyafanya hapa? Kwa maana wameijaza nchi hii udhalimu, tena wamerejea nyuma ili kunikasirisha; na, tazama, wanaliweka tawi puani.


Ndipo akaniambia, Uovu wa nyumba ya Israeli na Yuda ni mwingi sana, nayo nchi imejaa damu, nao mji umejaa kupotosha hukumu; maana husema, BWANA ameiacha nchi hii, naye BWANA haoni.


Kisha itakuwa wakati ule, nitauchunguza Yerusalemu kwa taa; nami nitawaadhibu watu walioganda juu ya masira yao; wasemao katika mioyo yao, BWANA hatatenda mema, wala hatatenda mabaya.


kwa kuwa yanayotendeka kwao kwa siri, ni aibu hata kuyanena.


Na alaaniwe mtu afanyaye sanamu ya kuchonga, au ya kusubu, machukizo kwa BWANA, kazi ya mikono ya fundi, akaisimamisha kwa siri. Na watu wote wajibu, waseme, Amina.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo