Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Ezekieli 7:13 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC

13 Kwa maana auzaye hatakirudia kilichouzwa, wajapokuwa wangali hai; kwa sababu maono haya yawahusu watu wote; hapana mmoja atakayerudi; wala hapana mtu atakayejitia nguvu katika uovu wa maisha yake.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

13 Wauzaji hawataweza kurudia mali yao waliyouza hata kama wakibaki hai. Kwani maono haya yahusu umati wote na hayatabatilishwa. Kutokana na uovu huo, hakuna mtu atakayesalimisha maisha yake.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

13 Wauzaji hawataweza kurudia mali yao waliyouza hata kama wakibaki hai. Kwani maono haya yahusu umati wote na hayatabatilishwa. Kutokana na uovu huo, hakuna mtu atakayesalimisha maisha yake.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

13 Wauzaji hawataweza kurudia mali yao waliyouza hata kama wakibaki hai. Kwani maono haya yahusu umati wote na hayatabatilishwa. Kutokana na uovu huo, hakuna mtu atakayesalimisha maisha yake.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

13 Muuzaji hatajipatia tena ardhi aliyoiuza wakati wote wawili wangali hai. Kwa kuwa maono kuhusu kundi lote hayatatanguka. Kwa sababu ya dhambi zao, hakuna hata mmoja atakayeokoa maisha yake.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

13 Muuzaji hatajipatia tena ardhi aliyoiuza wakati wote wawili wangali hai, kwa kuwa maono kuhusu kundi lote hayatatanguka. Kwa sababu ya dhambi zao, hakuna hata mmoja atakayeokoa maisha yake.

Tazama sura Nakili




Ezekieli 7:13
11 Marejeleo ya Msalaba  

Basi nanyi pia waandikieni Wayahudi vyovyote mpendavyo, kwa jina la mfalme, mkatie mhuri kwa pete ya mfalme; kwa kuwa andiko lililoandikwa kwa jina la mfalme na kutiwa mhuri kwa pete ya mfalme, hakuna awezaye kulitangua.


Kwa kuwa amenyosha mkono wake juu ya Mungu, Na kuendelea kwa kiburi kinyume cha Mwenyezi;


Kumbe! Huyu ndiye mtu yule, Asiyemfanya Mungu kuwa kimbilio lake. Aliutumainia wingi wa mali zake, Na kufanya mali kimbilio lake.


Hakuna mwenye uwezo juu ya roho aizuie roho; Wala hana mamlaka juu ya siku ya kufa; Wala hakuna kuponyoka katika vita vile; Wala uovu hautamwokoa yule aliyeuzoea.


Maana mimi ni BWANA; mimi nitanena, na neno lile nitakalolinena litatimizwa; wala halitakawilishwa tena; maana katika siku zenu, Ewe nyumba iliyoasi, nitalinena neno hilo na kulitimiza, asema Bwana MUNGU.


Basi uwaambie, Bwana MUNGU asema hivi; Maneno yangu hayatakawilishwa tena hata moja, bali neno nitakalolinena litatimizwa, asema Bwana MUNGU.


Kwa kuwa ninyi mmemhuzunisha moyo mwenye haki kwa uongo, ambaye mimi sikumhuzunisha; na kuitia nguvu mikono ya mtu mbaya, hata asigeuke, na kuiacha njia yake mbaya, na kuhifadhika;


Mwaka huo wa jubilii mtairudia kila mtu milki yake.


Lakini nyumba za vijiji, ambavyo havikuzingirwa na kuta, zitahesabiwa pamoja na mashamba ya nchi; nazo zina ruhusa ya kukombolewa, nazo zitatoka katika jubilii.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo