Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Ezekieli 48:15 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC

15 Na mianzi elfu tano iliyosalia katika upana, kuikabili hiyo elfu ishirini na tano, itatumiwa na watu wote, kwa huo mji, na kwa maskani, na kwa viunga, na huo mji utakuwa katikati yake.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

15 Ile sehemu ya eneo maalumu iliyobaki, yenye urefu wa kilomita kumi na mbili u nusu na upana kilomita 2.5, hilo ni kwa matumizi ya kawaida ya mji: Mahali pa kuishi na eneo la mashamba. Katikati yake kutakuwa na mji,

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

15 Ile sehemu ya eneo maalumu iliyobaki, yenye urefu wa kilomita kumi na mbili u nusu na upana kilomita 2.5, hilo ni kwa matumizi ya kawaida ya mji: Mahali pa kuishi na eneo la mashamba. Katikati yake kutakuwa na mji,

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

15 Ile sehemu ya eneo maalumu iliyobaki, yenye urefu wa kilomita kumi na mbili u nusu na upana kilomita 2.5, hilo ni kwa matumizi ya kawaida ya mji: mahali pa kuishi na eneo la mashamba. Katikati yake kutakuwa na mji,

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

15 “Eneo linalobaki lenye upana wa dhiraa elfu tano, na urefu wa dhiraa elfu ishirini na tano litakuwa kwa ajili ya matumizi ya kawaida ya mji, kwa ajili ya ujenzi wa nyumba na maeneo ya malisho. Mji utakuwa katikati yake

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

15 “Eneo linalobaki lenye upana wa dhiraa 5,000 na urefu wa dhiraa 25,000, litakuwa kwa ajili ya matumizi ya kawaida ya mji, kwa ajili ya ujenzi wa nyumba na malisho. Mji utakuwa katikati yake

Tazama sura Nakili




Ezekieli 48:15
5 Marejeleo ya Msalaba  

Makuhani wake wameivunja sheria yangu, wametia unajisi vitu vyangu vitakatifu; hawakuweka tofauti ya vitu vitakatifu na vitu vya kutumiwa sikuzote; wala hawakuwafundisha watu kupambanua vitu vichafu na vitu vilivyo safi, nao wamefumba macho yao, wasiziangalie sabato zangu, nami nimetiwa unajisi kati yao.


Alipima pande zake zote nne; lilikuwa na ukuta pande zote, urefu wake mianzi mia tano, na upana wake mianzi mia tano, ili kupatenga mahali palipo patakatifu, na mahali ambapo ni pa watu wote.


Nao watawafundisha watu wangu tofauti iliyoko kati ya vitu vitakatifu na vitu vya kawaida, na kuwafundisha kupambanua kati ya yaliyo machafu na yaliyo safi.


Nanyi mtaiandika milki ya mji, upana wake elfu tano, na urefu wake elfu ishirini na tano, kandokando ya mahali palipotolewa, iwe sehemu takatifu; nayo itakuwa ya nyumba yote ya Israeli.


Lakini nikikawia, upate kujua jinsi iwapasavyo watu kuenenda katika nyumba ya Mungu, iliyo kanisa la Mungu aliye hai, nguzo na msingi wa kweli.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo