Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -

Ezekieli 48:10 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC

10 Maeneo hayo matakatifu yatakuwa kwa ajili ya makuhani; upande wa kaskazini urefu wake mianzi elfu ishirini na tano, na upande wa magharibi upana wake mianzi elfu kumi, na upande wa mashariki upana wake mianzi elfu kumi, na upande wa kusini urefu wake mianzi elfu ishirini na tano; na mahali patakatifu pa BWANA patakuwa katikati yake.

Tazama sura Nakili

Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

10 Makuhani watakuwa na eneo lao katika eneo hilo. Eneo hilo litakuwa na urefu wa kilomita kumi na mbili u nusu kutoka mashariki hadi magharibi, na kilomita 5 kutoka kaskazini hadi kusini. Maskani ya Mungu itakuwa katikati ya eneo hilo.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

10 Makuhani watakuwa na eneo lao katika eneo hilo. Eneo hilo litakuwa na urefu wa kilomita kumi na mbili u nusu kutoka mashariki hadi magharibi, na kilomita 5 kutoka kaskazini hadi kusini. Maskani ya Mungu itakuwa katikati ya eneo hilo.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

10 Makuhani watakuwa na eneo lao katika eneo hilo. Eneo hilo litakuwa na urefu wa kilomita kumi na mbili u nusu kutoka mashariki hadi magharibi, na kilomita 5 kutoka kaskazini hadi kusini. Maskani ya Mungu itakuwa katikati ya eneo hilo.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

10 Hii itakuwa ni sehemu takatifu kwa ajili ya makuhani. Itakuwa na urefu wa dhiraa elfu ishirini na tano upande wa kaskazini, upana wa dhiraa elfu kumi upande wa magharibi, dhiraa elfu kumi upande wa mashariki, na urefu wa dhiraa elfu ishirini na tano upande wa kusini. Katikati yake patakuwa mahali patakatifu pa Mwenyezi Mungu.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

10 Hii itakuwa ni sehemu takatifu kwa ajili ya makuhani. Itakuwa na urefu wa dhiraa 25,000 upande wa kaskazini, upana wa dhiraa 10,000 upande wa magharibi, dhiraa 10,000 upande wa mashariki na urefu wa dhiraa 25,000 upande wa kusini. Katikati yake patakuwa mahali patakatifu pa bwana.

Tazama sura Nakili

Ezekieli 48:10
8 Marejeleo ya Msalaba  

BWANA akamwambia Abramu, alipokwisha kutengana na Lutu, Inua sasa macho yako, ukatazame kutoka hapo ulipo, upande wa kaskazini, na wa kusini na wa mashariki na wa magharibi;

Nao watakuwa na urithi; mimi ni urithi wao; wala hamtawapa milki iwayo yote katika Israeli; mimi ni milki yao.

Hiyo ni sehemu takatifu ya nchi; itakuwa ya makuhani, wahudumu wa patakatifu, wakaribiao kumhudumia BWANA; nayo itakuwa mahali kwa nyumba zao, na patakatifu kwa mahali patakatifu.

Matoleo hayo, mtakayomtolea BWANA, urefu wake ni mianzi elfu ishirini na tano, na upana wake elfu kumi.

wala mkoba wa safari, wala kanzu mbili, wala viatu, wala fimbo; maana mfanyakazi astahili posho yake.

Tufuate:

Matangazo

Matangazo