Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -

Ezekieli 48:1 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC

1 Basi, haya ndiyo majina ya makabila hayo; toka mwisho wa pande za kaskazini, karibu na njia ya Hethloni, hadi maingilio ya Hamathi, hadi Hasar-enoni, penye mpaka wa Dameski, yaani, upande wa kaskazini karibu na Hamathi, watakuwa na upande wa mashariki, na upande wa magharibi; Dani fungu moja.

Tazama sura Nakili

Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

1 Haya ndiyo majina ya makabila na sehemu zao: Kuanzia mpaka wa kaskazini kwenye barabara ya Hethloni hadi kuingia Hamathi hadi mji wa Hazar-enoni (ulioko mpakani mwa Damasko na Hamathi upande wa kaskazini na kuendelea kutoka mashariki hadi magharibi), eneo hilo litakuwa la kabila la Dani.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

1 Haya ndiyo majina ya makabila na sehemu zao: Kuanzia mpaka wa kaskazini kwenye barabara ya Hethloni hadi kuingia Hamathi hadi mji wa Hazar-enoni (ulioko mpakani mwa Damasko na Hamathi upande wa kaskazini na kuendelea kutoka mashariki hadi magharibi), eneo hilo litakuwa la kabila la Dani.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

1 “Haya ndiyo majina ya makabila na sehemu zao: “Kwenye mpaka wa kaskazini, Dani atakuwa na sehemu moja; mpaka huo utafuata barabara ya Hethloni hadi Lebo-Hamathi; Hasar-Enani hata mpaka wa kaskazini wa Dameski karibu na Hamathi utakuwa sehemu ya huo mpaka wake kuanzia upande wa mashariki hadi upande wa magharibi.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

1 “Haya ndiyo majina ya makabila na sehemu zao: “Kwenye mpaka wa kaskazini, Dani atakuwa na sehemu moja, mpaka huo utafuata barabara ya Hethloni hadi Lebo-Hamathi, Hasar-Enani hata mpaka wa kaskazini wa Dameski karibu na Hamathi utakuwa sehemu ya huo mpaka wake kuanzia upande wa mashariki hadi upande wa magharibi.

Tazama sura Nakili

Ezekieli 48:1
16 Marejeleo ya Msalaba  

Basi mfalme akamwambia Yoabu, jemadari wa jeshi la askari, waliokuwa pamoja naye, Zunguka sasa katikati ya kabila zote za Israeli, tangu Dani mpaka Beer-sheba, mkawahesabu watu, nipate kujua idadi yao.

Bwana MUNGU asema hivi; Huu ndio mpaka ambao mtaigawanya nchi iwe urithi sawasawa na makabila kumi na mawili ya Israeli; kwa Yusufu, mafungu mawili.

Na upande wa magharibi, utakuwa ni bahari kubwa, kutoka mpaka wa kusini mpaka mahali penye kuelekea maingilio ya Hamathi. Huu ndio upande wa magharibi.

Tena itakuwa, mgeni akaaye katika kabila iwayo yote, atapewa urithi katika kabila asema Bwana MUNGU.

Huu ndio urithi wa kabila la wana wa Dani kwa kufuata jamaa zao; miji hii pamoja na vijiji vyake.

Tufuate:

Matangazo

Matangazo