Ezekieli 46:9 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC9 Lakini watu wa nchi watakapokuja mbele za BWANA katika sikukuu zilizoamriwa, yeye aingiaye kwa njia ya lango la upande wa kaskazini ili kuabudu, atatoka kwa njia ya lango la upande wa kusini; na yeye aingiaye kwa njia ya lango la upande wa kusini, atatoka kwa njia ya lango la upande wa kaskazini; hatarudi kwa njia ya lango aliloingia kwalo, lakini atatoka kwa kwenda mbele moja kwa moja. Tazama suraMatoleo zaidiBiblia Habari Njema9 Watu wanapokuja kumwabudu Mwenyezi-Mungu wakati wa sikukuu yoyote, wale walioingia kwa njia ya lango la kaskazini, watatoka kwa njia ya lango la kusini; na wale walioingia kwa lango la kusini, watatoka kwa njia ya lango la kaskazini. Mtu asirudi kwa njia ya lango aliloingilia, bali atatoka kwa njia ya lango lililo mbele yake. Tazama suraBiblia Habari Njema - BHND9 Watu wanapokuja kumwabudu Mwenyezi-Mungu wakati wa sikukuu yoyote, wale walioingia kwa njia ya lango la kaskazini, watatoka kwa njia ya lango la kusini; na wale walioingia kwa lango la kusini, watatoka kwa njia ya lango la kaskazini. Mtu asirudi kwa njia ya lango aliloingilia, bali atatoka kwa njia ya lango lililo mbele yake. Tazama suraBiblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza9 Watu wanapokuja kumwabudu Mwenyezi-Mungu wakati wa sikukuu yoyote, wale walioingia kwa njia ya lango la kaskazini, watatoka kwa njia ya lango la kusini; na wale walioingia kwa lango la kusini, watatoka kwa njia ya lango la kaskazini. Mtu asirudi kwa njia ya lango aliloingilia, bali atatoka kwa njia ya lango lililo mbele yake. Tazama suraNeno: Bibilia Takatifu9 “ ‘Watu wa nchi wanapokuja mbele za Mwenyezi Mungu katika sikukuu zilizoamriwa, yeyote aingiaye kwa lango la kaskazini kuabudu atatoka nje kwa lango la kusini; na yeyote aingiaye kwa lango la kusini atatoka nje kwa lango la kaskazini. Hakuna mtu yeyote atakayerudi kupitia lango lile aliloingilia, lakini kila mmoja atatoka nje kwa lango linalokabili lile aliloingilia. Tazama suraNeno: Maandiko Matakatifu9 “ ‘Wakati watu wa nchi wanapokuja mbele za bwana katika sikukuu zilizoamriwa, yeyote aingiaye kwa lango la kaskazini kuabudu atatoka nje kwa lango la kusini na yeyote aingiaye kwa lango la kusini atatoka nje kwa lango la kaskazini. Hakuna mtu yeyote atakayerudi kwa kupitia lango lile aliloingilia, lakini kila mmoja atatoka nje kwa lango linalokabili lile aliloingilia. Tazama sura |