Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -

Ezekieli 46:7 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC

7 Naye atatengeneza sadaka ya unga, efa moja kwa ng'ombe dume, na efa moja kwa kondoo dume, na kwa wale wana-kondoo, kwa kiasi awezacho kutoa, na hini moja ya mafuta kwa efa moja.

Tazama sura Nakili

Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

7 Pamoja na kila fahali na kila kondoo dume anayetolewa sadaka, ni lazima pawepo lita kumi na saba na nusu za unga, na pamoja na kila mwanakondoo, ni lazima pawepo chochote ambacho mtawala anatoa. Tena kwa kila sadaka ya nafaka, ni lazima kutoa lita tatu za nafaka.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

7 Pamoja na kila fahali na kila kondoo dume anayetolewa sadaka, ni lazima pawepo lita kumi na saba na nusu za unga, na pamoja na kila mwanakondoo, ni lazima pawepo chochote ambacho mtawala anatoa. Tena kwa kila sadaka ya nafaka, ni lazima kutoa lita tatu za nafaka.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

7 Atatoa sadaka ya nafaka ya: efa moja kwa huyo fahali, na efa moja kwa huyo kondoo dume; na kwa wana-kondoo atatoa nafaka nyingi kama atakavyo kutoa; atatoa hini ya mafuta kwa kila efa.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

7 Atatoa kuwa sadaka ya nafaka efa moja pamoja na fahali mmoja, efa moja na kondoo dume mmoja na pamoja na wana-kondoo kama atakavyo kutoa, pamoja na hini ya mafuta kwa kila efa.

Tazama sura Nakili

Ezekieli 46:7
6 Marejeleo ya Msalaba  

Naye atatengeneza sadaka ya unga, efa moja kwa ng'ombe, na efa moja kwa kondoo dume, na hini moja ya mafuta kwa efa moja;

Na katika sikukuu hizo, na sikukuu nyingine zilizoamriwa, sadaka ya unga itakuwa efa moja kwa ng'ombe mmoja, na efa moja kwa kondoo dume mmoja, na kwa wale wana-kondoo kiasi awezacho kutoa, na hini moja ya mafuta kwa efa moja.

Na sadaka ya unga itakuwa efa moja kwa kondoo dume, na sadaka ya unga kwa wale wana-kondoo, kiasi awezacho kutoa, na hini moja ya mafuta kwa efa moja.

Lakini akiwa ni maskini, naye hawezi kupata kiasi hicho, ndipo atatwaa mwana-kondoo mmoja wa kiume, awe sadaka ya hatia ya kutikiswa, ili kufanya upatanisho kwa ajili yake, na sehemu ya kumi ya efa ya unga mwembamba, uliochanganywa na mafuta kuwa sadaka ya unga, na logi ya mafuta;

Tena katika mianzo ya miezi yenu mtamsogezea BWANA sadaka ya kuteketezwa; nayo ni ng'ombe dume wadogo wawili, na kondoo dume mmoja, na wana-kondoo wa kiume wa mwaka wa kwanza, wakamilifu, saba;

Kila mtu na atoe kama awezavyo, kwa kadiri ya baraka ya BWANA, Mungu wako, alivyokupa.

Tufuate:

Matangazo

Matangazo