Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Ezekieli 46:5 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC

5 Na sadaka ya unga itakuwa efa moja kwa kondoo dume, na sadaka ya unga kwa wale wana-kondoo, kiasi awezacho kutoa, na hini moja ya mafuta kwa efa moja.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

5 Pamoja na kila kondoo dume, ataleta sadaka ya unga lita kumi na saba na nusu, lakini pamoja na kila mwanakondoo ataleta sadaka yoyote anayoweza. Na kwa kila sadaka ya unga, ataleta lita tatu za mafuta.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

5 Pamoja na kila kondoo dume, ataleta sadaka ya unga lita kumi na saba na nusu, lakini pamoja na kila mwanakondoo ataleta sadaka yoyote anayoweza. Na kwa kila sadaka ya unga, ataleta lita tatu za mafuta.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

5 Pamoja na kila kondoo dume, ataleta sadaka ya unga lita kumi na saba na nusu, lakini pamoja na kila mwanakondoo ataleta sadaka yoyote anayoweza. Na kwa kila sadaka ya unga, ataleta lita tatu za mafuta.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

5 Sadaka ya nafaka inayotolewa pamoja na huyo kondoo dume itakuwa efa moja, na sadaka ya nafaka inayotolewa na hao wana-kondoo itakuwa kiasi apendacho mtu pamoja na hini ya mafuta kwa kila efa.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

5 Sadaka ya nafaka inayotolewa pamoja na huyo kondoo dume itakuwa efa moja na sadaka ya nafaka inayotolewa na hao wana-kondoo itakuwa kiasi apendacho mtu pamoja na hini ya mafuta kwa kila efa.

Tazama sura Nakili




Ezekieli 46:5
7 Marejeleo ya Msalaba  

Naye atatengeneza sadaka ya unga, efa moja kwa ng'ombe, na efa moja kwa kondoo dume, na hini moja ya mafuta kwa efa moja;


Naye atatengeneza sadaka ya unga, efa moja kwa ng'ombe dume, na efa moja kwa kondoo dume, na kwa wale wana-kondoo, kwa kiasi awezacho kutoa, na hini moja ya mafuta kwa efa moja.


Lakini akiwa ni maskini, naye hawezi kupata kiasi hicho, ndipo atatwaa mwana-kondoo mmoja wa kiume, awe sadaka ya hatia ya kutikiswa, ili kufanya upatanisho kwa ajili yake, na sehemu ya kumi ya efa ya unga mwembamba, uliochanganywa na mafuta kuwa sadaka ya unga, na logi ya mafuta;


pamoja na sehemu ya kumi tatu za efa za unga mwembamba kuwa sadaka ya unga, uliochanganywa na mafuta, kwa kila ng'ombe; na sehemu ya kumi mbili za unga mwembamba kuwa sadaka ya unga, uliochanganywa na mafuta, kwa huyo kondoo dume mmoja;


Sheria ya Mnadhiri awekaye nadhiri ni hiyo, tena ni sheria ya sadaka yake atakayomtolea BWANA kwa ajili ya kujitenga kwake, pamoja na vitu vile ambavyo aweza kuvipata zaidi; kama nadhiri yake awekayo ilivyo, ndivyo impasavyo kufanya kwa kuifuata sheria ya kujitenga kwake.


Kila mtu na atoe kama awezavyo, kwa kadiri ya baraka ya BWANA, Mungu wako, alivyokupa.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo