Ezekieli 46:2 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC2 Naye mkuu ataingia kwa njia ya ukumbi wa lango lile, upande wa nje, naye atasimama karibu na mwimo wa lango, nao makuhani wataitengeneza sadaka yake ya kuteketezwa, na sadaka zake za amani, naye ataabudu penye kizingiti cha lango; kisha atatoka; lakini lango lile halitafungwa hadi wakati wa jioni. Tazama suraMatoleo zaidiBiblia Habari Njema2 Toka nje, mtawala ataingia ukumbi wa ndani kwa kupitia lango la ukumbi huo. Naye atasimama karibu na nguzo ya lango, wakati makuhani wanateketeza sadaka zake za kuteketezwa na sadaka za amani. Kisha mtawala huyo atasujudia kwenye lango na baadaye atatoka nje. Lango litabaki wazi hadi jioni. Tazama suraBiblia Habari Njema - BHND2 Toka nje, mtawala ataingia ukumbi wa ndani kwa kupitia lango la ukumbi huo. Naye atasimama karibu na nguzo ya lango, wakati makuhani wanateketeza sadaka zake za kuteketezwa na sadaka za amani. Kisha mtawala huyo atasujudia kwenye lango na baadaye atatoka nje. Lango litabaki wazi hadi jioni. Tazama suraBiblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza2 Toka nje, mtawala ataingia ukumbi wa ndani kwa kupitia lango la ukumbi huo. Naye atasimama karibu na nguzo ya lango, wakati makuhani wanateketeza sadaka zake za kuteketezwa na sadaka za amani. Kisha mtawala huyo atasujudia kwenye lango na baadaye atatoka nje. Lango litabaki wazi hadi jioni. Tazama suraNeno: Bibilia Takatifu2 Mkuu anayetawala ataingia kupitia baraza ya njia ya lango la ukumbi na kusimama karibu na nguzo ya lango. Makuhani watatoa sadaka za mkuu anayetawala za kuteketezwa na sadaka za amani. Mkuu anayetawala atasujudu kwenye kizingiti cha njia ya lango, kisha atatoka nje, lakini lango halitafungwa hadi jioni. Tazama suraNeno: Maandiko Matakatifu2 Mkuu anayetawala ataingia kupitia baraza ya njia ya lango la ukumbi na kusimama karibu na nguzo ya lango. Makuhani watatoa sadaka za mkuu anayetawala za kuteketezwa na sadaka za amani. Mkuu anayetawala atasujudu kwenye kizingiti cha njia ya lango, kisha atatoka nje, lakini lango halitafungwa mpaka jioni. Tazama sura |
Naye mkuu atakapotengeneza sadaka atoayo kwa hiari yake mwenyewe, sadaka ya kuteketezwa, au sadaka za amani, ziwe sadaka amtoleazo BWANA kwa hiari yake mwenyewe, mtu mmoja atamfungulia lango lile lielekealo upande wa mashariki, naye ataitoa sadaka yake ya kuteketezwa, na sadaka zake za amani, kama afanyavyo siku ya sabato; kisha atatoka; na baada ya kutoka kwake mtu mmoja atalifunga lango.