Ezekieli 46:1 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC1 Bwana MUNGU asema hivi; Lango la ua wa ndani, lielekealo upande wa mashariki litafungwa siku sita za kazi; lakini siku ya sabato litafunguliwa, na siku ya mwezi mwandamo litafunguliwa. Tazama suraMatoleo zaidiBiblia Habari Njema1 “Mimi Bwana Mwenyezi-Mungu nasema hivi: Lango la ua wa ndani unaoelekea mashariki litafungwa siku zote sita za kazi. Siku za sabato na siku za mwezi mwandamo litafunguliwa. Tazama suraBiblia Habari Njema - BHND1 “Mimi Bwana Mwenyezi-Mungu nasema hivi: Lango la ua wa ndani unaoelekea mashariki litafungwa siku zote sita za kazi. Siku za sabato na siku za mwezi mwandamo litafunguliwa. Tazama suraBiblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza1 “Mimi Bwana Mwenyezi-Mungu nasema hivi: Lango la ua wa ndani unaoelekea mashariki litafungwa siku zote sita za kazi. Siku za sabato na siku za mwezi mwandamo litafunguliwa. Tazama suraNeno: Bibilia Takatifu1 “ ‘Hili ndilo asemalo Bwana Mungu Mwenyezi: Lango la ukumbi wa ndani linaloelekea upande wa mashariki litakuwa linafungwa kwa siku sita za juma, ila siku ya Sabato na siku ya Mwezi Mwandamo litafunguliwa. Tazama suraNeno: Maandiko Matakatifu1 “ ‘Hili ndilo bwana Mwenyezi asemalo: Lango la ukumbi wa ndani linaloelekea upande wa mashariki litakuwa linafungwa kwa siku sita za juma, ila siku ya Sabato na siku ya Mwezi Mwandamo litafunguliwa. Tazama sura |
Naye mkuu atakapotengeneza sadaka atoayo kwa hiari yake mwenyewe, sadaka ya kuteketezwa, au sadaka za amani, ziwe sadaka amtoleazo BWANA kwa hiari yake mwenyewe, mtu mmoja atamfungulia lango lile lielekealo upande wa mashariki, naye ataitoa sadaka yake ya kuteketezwa, na sadaka zake za amani, kama afanyavyo siku ya sabato; kisha atatoka; na baada ya kutoka kwake mtu mmoja atalifunga lango.