Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Ezekieli 45:5 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC

5 Tena urefu wa elfu ishirini na tano, na upana wa elfu kumi, ni sehemu ya Walawi, wahudumu wa nyumba, iwe milki yao wenyewe kwa vyumba ishirini.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

5 Eneo lingine lenye urefu wa kilomita kumi na mbili u nusu kwa kilomita tano, litatengwa kwa ajili ya miji ya Walawi wanaohudumu hekaluni liwe milki yao.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

5 Eneo lingine lenye urefu wa kilomita kumi na mbili u nusu kwa kilomita tano, litatengwa kwa ajili ya miji ya Walawi wanaohudumu hekaluni liwe milki yao.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

5 Eneo lingine lenye urefu wa kilomita kumi na mbili u nusu kwa kilomita tano, litatengwa kwa ajili ya miji ya Walawi wanaohudumu hekaluni liwe milki yao.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

5 Eneo la urefu wa dhiraa elfu ishirini na tano, na upana wa dhiraa elfu kumi litakuwa la Walawi, wanaohudumu hekaluni, kama milki yao kwa ajili ya miji ya kuishi.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

5 Eneo la urefu wa dhiraa 25,000 na upana wa dhiraa 10,000 litakuwa la Walawi wale wanaotumika hekaluni, kama milki yao kwa ajili ya miji ya kuishi.

Tazama sura Nakili




Ezekieli 45:5
9 Marejeleo ya Msalaba  

Ndipo akanileta mpaka katika ua wa nje, na tazama, palikuwa na vyumba, na sakafu iliyofanyizwa kwa ule ua pande zote; vyumba thelathini vilikuwako juu ya sakafu ile.


Maeneo hayo matakatifu yatakuwa kwa ajili ya makuhani; upande wa kaskazini urefu wake mianzi elfu ishirini na tano, na upande wa magharibi upana wake mianzi elfu kumi, na upande wa mashariki upana wake mianzi elfu kumi, na upande wa kusini urefu wake mianzi elfu ishirini na tano; na mahali patakatifu pa BWANA patakuwa katikati yake.


Na kuukabili mpaka wa makuhani, Walawi watakuwa na fungu, urefu wake mianzi elfu ishirini na tano, na upana wake mianzi elfu kumi; urefu wote utakuwa mianzi elfu ishirini na tano, na upana wake mianzi elfu kumi.


Matoleo yote yatakuwa mianzi elfu ishirini na tano, kwa mianzi elfu ishirini na tano; mtatoa matoleo matakatifu, nchi ya mraba, pamoja na milki ya mji.


Mtakaa katika vibanda muda wa siku saba; wazaliwa wote wa Israeli watakaa katika vibanda;


Uwaagize wana wa Israeli wawape Walawi miji wapate mahali pa kukaa, katika milki yao; pamoja na malisho yaliyoizunguka hiyo miji kotekote mtawapa Walawi.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo