Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Ezekieli 45:4 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC

4 Hiyo ni sehemu takatifu ya nchi; itakuwa ya makuhani, wahudumu wa patakatifu, wakaribiao kumhudumia BWANA; nayo itakuwa mahali kwa nyumba zao, na patakatifu kwa mahali patakatifu.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

4 Eneo hilo litakuwa takatifu nchini, na kutengwa kwa ajili ya makuhani wanaomtumikia Mwenyezi-Mungu katika maskani yake. Ndani ya eneo hilo kutakuwa na nyumba zao na nafasi iliyowekwa wakfu kwa ajili ya maskani yangu.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

4 Eneo hilo litakuwa takatifu nchini, na kutengwa kwa ajili ya makuhani wanaomtumikia Mwenyezi-Mungu katika maskani yake. Ndani ya eneo hilo kutakuwa na nyumba zao na nafasi iliyowekwa wakfu kwa ajili ya maskani yangu.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

4 Eneo hilo litakuwa takatifu nchini, na kutengwa kwa ajili ya makuhani wanaomtumikia Mwenyezi-Mungu katika maskani yake. Ndani ya eneo hilo kutakuwa na nyumba zao na nafasi iliyowekwa wakfu kwa ajili ya maskani yangu.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

4 Itakuwa sehemu takatifu ya nchi kwa ajili ya makuhani, wale wanaohudumu ndani ya mahali patakatifu na ambao hukaribia ili kuhudumu mbele za Mwenyezi Mungu. Patakuwa mahali pa nyumba zao pamoja na sehemu kwa ajili ya mahali patakatifu.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

4 Itakuwa sehemu takatifu ya nchi kwa ajili ya makuhani, wale wanaohudumu ndani ya mahali patakatifu na ambao hukaribia ili kuhudumu mbele za bwana. Patakuwa mahali pa nyumba zao pamoja na sehemu kwa ajili ya mahali patakatifu.

Tazama sura Nakili




Ezekieli 45:4
10 Marejeleo ya Msalaba  

Akaniambia, Chumba hiki kinachokabili upande wa kusini ni kwa ajili ya makuhani, yaani, hao wasimamizi wa nyumba.


Nacho chumba kinachokabili upande wa kaskazini ni cha makuhani, wasimamizi wa madhabahu; hao ni wana wa Sadoki, ambao kati ya wana wa Lawi, ndio waliomkaribia BWANA, ili kumtumikia.


Utawapa makuhani Walawi, walio wa uzao wa Sadoki, walio karibu nami, ili kunihudumu, asema Bwana MUNGU, ng'ombe dume mchanga awe sadaka ya dhambi.


Nao watakuwa na urithi; mimi ni urithi wao; wala hamtawapa milki iwayo yote katika Israeli; mimi ni milki yao.


Tena, mtakapoigawanya nchi kwa kura iwe urithi, mtamtolea BWANA toleo, sehemu takatifu ya nchi, urefu wake utakuwa urefu wa mianzi elfu ishirini na tano, na upana wake elfu kumi; itakuwa takatifu ndani ya mipaka yake yote pande zote.


Na kwa kipimo hicho utapima, urefu wa elfu ishirini na tano, na upana wa elfu kumi; na ndani yake patakuwa patakatifu, palipo patakatifu sana.


Na mpakani mwa Yuda, toka upande wa mashariki hadi upande wa magharibi, yatakuwapo matoleo mtakayotoa, upana wake mianzi elfu ishirini na tano, na urefu wake sawasawa na moja la mafungu hayo, toka upande wa mashariki hadi upande wa magharibi; na mahali patakatifu ni katikati yake.


kisha akanena na Kora na mkutano wake wote, akawaambia, Asubuhi BWANA ataonesha ni kina nani walio wake, kisha ni nani aliye mtakatifu, tena ni nani atakayemkaribisha kwake; maana, yeye atakayemchagua ndiye atakayemsongeza kwake.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo