Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Ezekieli 45:15 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC

15 na mwana-kondoo mmoja wa kundi katika mia mbili, katika malisho ya Israeli yenye maji; kwa sadaka ya unga, na kwa sadaka ya kuteketezwa, na kwa sadaka za amani, ili kuwafanyia upatanisho, asema Bwana MUNGU.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

15 Watatoa kondoo mmoja kwa kila kundi la kondoo 200 katika jamaa za Israeli. Wataleta sadaka za nafaka, sadaka za kuteketezwa, na sadaka za amani, ili wapate kufanyiwa upatanisho. Mimi Bwana Mwenyezi-Mungu nimesema.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

15 Watatoa kondoo mmoja kwa kila kundi la kondoo 200 katika jamaa za Israeli. Wataleta sadaka za nafaka, sadaka za kuteketezwa, na sadaka za amani, ili wapate kufanyiwa upatanisho. Mimi Bwana Mwenyezi-Mungu nimesema.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

15 Watatoa kondoo mmoja kwa kila kundi la kondoo 200 katika jamaa za Israeli. Wataleta sadaka za nafaka, sadaka za kuteketezwa, na sadaka za amani, ili wapate kufanyiwa upatanisho. Mimi Bwana Mwenyezi-Mungu nimesema.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

15 Pia kondoo mmoja atachukuliwa kutoka kila kundi la kondoo mia mbili katika malisho yenye maji mengi ya Israeli. Hivi vitatumika kwa ajili ya sadaka ya nafaka, sadaka ya kuteketezwa na sadaka za amani ili kufanya upatanisho kwa ajili ya watu, asema Bwana Mungu Mwenyezi.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

15 Pia kondoo mmoja atachukuliwa kutoka kwenye kila kundi la kondoo mia mbili kutoka kwenye malisho yaliyonyeshewa vizuri ya Israeli. Hivi vitatumika kwa ajili ya sadaka ya nafaka, sadaka ya kuteketezwa na sadaka za amani ili kufanya upatanisho kwa ajili ya watu, asema bwana Mwenyezi.

Tazama sura Nakili




Ezekieli 45:15
15 Marejeleo ya Msalaba  

na sehemu ya mafuta iliyoamriwa, katika bathi ya mafuta, itakuwa sehemu ya kumi ya bathi katika kori moja, ambayo ni bathi kumi, yaani homeri; maana bathi kumi ni homeri moja;


Tena itakuwa kazi ya mkuu kutoa hizo sadaka za kuteketezwa, na sadaka za unga, na sadaka za vinywaji, katika sikukuu, na katika mwezi mpya, na katika sabato, katika sikukuu zote za nyumba ya Israeli zilizoamriwa; atatengeneza sadaka ya dhambi, na sadaka ya unga, na sadaka ya kuteketezwa, na sadaka za amani, ili kufanya upatanisho kwa ajili ya nyumba ya Israeli.


Nawe utafanya vivyo hivyo katika mwezi wa saba, siku ya kwanza ya mwezi kwa ajili ya kila mtu akosaye, na kwa ajili ya mtu aliye mjinga, ndivyo mtakavyoifanyia nyumba upatanisho.


Muda wa majuma sabini umeamriwa juu ya watu wako, na juu ya mji wako mtakatifu, ili kukomesha makosa, na kumaliza dhambi, na kufanya upatanisho kwa ajili ya uovu, na kuleta haki ya milele, na kutia mhuri maono na unabii, na kumtia mafuta yeye aliye mtakatifu.


Kisha ataweka mkono wake juu ya kichwa cha hiyo sadaka ya kuteketezwa; nayo itakubaliwa kwa ajili yake, ili kufanya upatanisho kwa ajili yake.


Wala haitaliwa sadaka ya dhambi yoyote, ambayo damu yake yoyote ililetwa ndani ya hema ya kukutania, ili kufanya upatanisho katika mahali patakatifu; itateketezwa.


Lakini na alaaniwe mtu adanganyaye, ambaye katika kundi lake ana dume, akaweka nadhiri, ila amtolea Bwana kitu kilicho na kilema; kwa maana mimi ni Mfalme mkuu, asema BWANA wa majeshi, na jina langu latisha katika mataifa.


Tena mtoapo sadaka aliye kipofu, si vibaya? Na mtoapo sadaka walio vilema na wagonjwa, si vibaya? Haya! Mtolee mtawala wako; Je, Atakuwa radhi nawe? Au atakukubali nafsi yako? Asema BWANA wa majeshi.


Kwa maana ikiwa tulipokuwa adui tulipatanishwa na Mungu kwa mauti ya Mwana wake; zaidi sana baada ya kupatanishwa tutaokolewa katika uzima wake.


Akawapatanisha wote wawili na Mungu katika mwili mmoja, kwa njia ya msalaba, akiisha kuumaliza ule uadui kwa huo msalaba.


Na ninyi, mliokuwa hapo kwanza mmetengwa, tena adui katika nia zenu, kwa matendo yenu mabaya, amewapatanisha sasa;


Hivyo ilimpasa kufananishwa na ndugu zake katika mambo yote, apate kuwa kuhani mkuu mwenye rehema, mwaminifu katika mambo ya Mungu, ili afanye kafara ya suluhu kwa dhambi za watu wake.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo